Picha Kutoka Eneo la Ajali ya Ndege iliyoua watu 11 Ngorongoro Arusha
Jeshi la Polisi Arusha limepata miili ya watu 11 waliofariki kwenye ajali ya ndege ndogo ya Coastal Aviation iliyotokea November 15, 2017 katika eneo la Embakazi Wilayani Ngorongoro.
Ndege hiyo ilipaa kutoka uwanja mdogo wa Arusha saa nne na dakika 10 asubuhi kuelekea uwanja wa Ndege Kilimanjaro (KIA) na kuchukua abiria watano jumla ikawa na abiria 10 na Rubani akiwa ni mtu wa 11 kwenye ndege hiyo na kuelekea Ngorongoro.
Maoni