Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya WANAUME

Utafiti: Wanawake wa Rwanda na Kenya ndio wataishi muda mrefu zaidi Afrika Mashariki

Wanawake nchini Rwanda na Kenya ndio wanaotarajiwa kuishi muda mrefu zaidi miongoni mwa wanawake na wanaume katika nchi za Afrika Mashariki, kwa mujibu wa takwimu. Umri wa wanawake kuishi Rwanda kwa sasa ni miaka 69.3 na nchini Kenya ni miaka 69.0. Hata hivyo, umri wa kuishi wa wanaume Uganda ndio ulioongezeka zaidi katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, ambapo umepanda kwa miaka 13.5. Nchini Tanzania, umri wa kawaida wa kuishi kwa wanawake kufikia mwaka 2016 ulikuwa miaka 66, ongezeko la miaka 10 ukilinganisha na mwaka 1990 kwa mujibu wa Utafiti wa Mzigo wa Maradhi Duniani mwaka 2016, ulioratibiwa na Taasisi ya Takwimu za Afya na Utathmini. Kwa wanaume, umri wa kuishi ulikuwa miaka 62.6 kufikia mwaka 2016 ukilinganisha na miaka 53.7 mwaka 1990. Kwa kiwango cha kadiri, umri wa kuishi kwa Watanzania umeongezeka kwa miaka kumi kufikia sasa tangu mwaka 1990. Nchini Kenya, umri wa kuishi kwa wanawake umeongezeka kutoka miaka 62.6 mwaka 1990 hadi miaka 69 mwaka 2016,...