Alexandre Lacazette Atletico Madrid wanataka kumsajili Alexandre Lacazette kuchukua nafasi ya mshambuliaji Antoine Griezmann, 28 ambaye anaelekea Barcelona. (Mirror) United watalazimika kilipa zaidi ya pauni milioni £90 kumnunua beki wa Leicester City na England, Harry Maguire - hatua itakayomfanya kuwa nyota huyo wa miaka 26 kuwa mlinzi ghali zaidi . (Telegraph) United pia imetuma maombi ya kumnasa kiungo wa kati wa Uhispania na Dinamo Zagreb-Dani Olmo, 21. (Mail) Real Madrid wana mpango wa kumjumuisha mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, katika mkataba utakaowawezesha kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mail) Gareth Bale Mlinzi wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24, huenda akatia saini mkataba wa kujiunga na Manchester City mhumu ujao. (L'Equipe, via Manchester Evening News) Crystal Palace wanafanya kila juhudi kuhakikisha hawataiuzia Arsenal winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, na wana hasiri kwa sababu wanaamini G...