Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 30.10.2018

: Mauricio Pochettino, Antonio Conte, Loris Karius, Divock Origi, Jose Mourinho, Ousmane Dembele, Cristiano Ronaldo




Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 33, amesema aliihama Real Madrid na kujiunga na Juventus kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Uhispania Florentino Perez hakumfanya ajihisi kama mchezaji anayethaminiwa na kudhaminiwa sana. (L'Equipe, kupitia Express)


Real Madrid wanamtaka meneja wa sasa wa Tottenham Mauricio Pochettino awe meneja wao mpya wa kudumu kufikia mwisho wa mwezi huu. Miamba hao wa Uhispania walimfuta kazi Julen Lopetegui baada yake kuhudumu kwa miezi minne na nusu Jumatatu. Alifutwa baada ya Madrid kuchapwa 5-1 na Barcelona Jumapili. (Sun)


Mazungumzo ya Real na kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ya kumtaka achukue mikoba ya ukufunzi Madrid yamekwama. Hii ndiyo sababu iliyochangia Santiago Solari ambaye ni mkufunzi wa timu ya akiba kuwekwa kwenye usukani. Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu pia kumrithi Lopetegui. (Marca)


Antonio Conte

Besiktas wanataka kumrejesha kipa wa Liverpool Loris Karius kwa klabu hiyo ya Anfield. Kocha huyo alitia saini mkataba wa mkopo wa miaka miwili na klabu hiyo ya Uturuki.

Samatta afunga magoli mawili Europa League


Wanataka Mjerumani huyo arejee Anfield mwezi januari na badala yake wakabidhiwe mshambuliaji Mbelgiji mwenye asili ya Kenya Divock Origi, 23. (90 Minutes)


Karius alifungwa mabao manne Europa League na KRC Genk

Meneja Jose Mourinho ataungwa mkono Januari kuwanunua wachezaji zaidi kuimarisha kikosi cha Manchester United iwapo atawapata wachezaji wafaao. Inadaiwa kwamba ametengewa kitita cha karibu Ā£100m. (Guardian)

Mwanawe Vichai Srivaddhanaprabha, Aiyawatt, aliyekuwa wa kwanza kumhoji meneja Claudio Ranieri aliyewasaidia kushinda Ligi Kuu ya England kabla yake kuteuliwa rasmi, anatarajiwa kuongoza Leicester baada ya babake kufariki katika ajali ya helikopta iliyoua babake na watu wengine wanne. (Mail)

Mshambuliaji wa Barcelona anayechezea Ufaransa Ousmane Dembele huenda akaruhusiwa kuondoka klabu hiyo mwezi Januari. Chelsea, Liverpool na Arsenal ni miongoni mwa klabu ambazo zimehusishwa na kutaka kumchukua mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Sun)


Dembele alinunuliwa Ā£96.8m na Barca mwaka jana, ada ambayo ilitarajiwa kupanda hadi Ā£135.5m

Juventus wanataka sana kumnunua beki wa miaka 21 kutoka Serbia Nikola Milenkovic, ambaye anadaiwa pia kunyatiwa na Tottenham na Manchester United. Juve pia wanamtaka kiungo wa kati wa Italia Federico Chiesa, 21, lakini Fiorentina huenda wakataka kulipwa zaidi ya euro 100m (Ā£89m) ndipo wakubali kuwaachilia wawili hao. (Calciomercato)

Meneja wa zamani wa Aston Villa Steve Bruce anahusishwa na kuhamia Reading. Klabu hiyo kwa sasa inashikilia nafasi ya 22 kwenye liig ya wakiwa na Paul Clement. (Birmingham Mail)


Meneja wa Bournemouth Eddie Howe amemhakikishia mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya England Jermain Defoe kwamba bado anahitajika Bournemouth, licha ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 36 kuchezeshwa mara tatu pekee Ligi ya Premia, wakati wote akiingia kama nguvu mpya. (Mirror)

Manchester United hawajawasiliana na mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig Paul Mitchell kuhusu kuhudumu katika nafasi kama hiyo ambayo wanapanga kuianzisha Old Trafford. Hata hivyo, mkuu huyo wa zamani wa usajili wa wachezaji Tottenham anafurahia kuhusishwa na kazi hiyo. (Sun)


Jermain Defoe alikuwa na urafiki na Bradley Lowery kabla ya mtoto huyo kufariki Julai 2017 kutokana na saratani

Kiungo wa kati wa Liverpool kutoka Brazil Fabinho, 25, anasema amekubwa na matatizo katika kujaribu kuzoea maisha mapya tangu alipohamia Anfield kutoka Monaco kwa Ā£39m majira yajoto. (ESPN)


Memphis Depay

Winga wa Lyon na Uholanzi aliyewahi kuichezea Manchester United Memphis Depay, 24, amedai kwamba hajajihisi kama mchezaji anayeheshimiwa. (ESPN)


Fabinho akisherehekea kufunga bao alipokuwa Monaco

Meneja wa Rafael Benitez amesisitiza kwamba Newcastle ni mkosi tu unaowaandama na si kwamba hawachezi vyema kwenye mechi zao za karibuni. Vijana hao wameshindwa kushinda mechi hata moja kati ya kumi za kwanza walizocheza msimu huu. (Newcastle Chronicle)

Meneja wa Aston Villa Dean Smith anapanga kuwasilisha ofa ya Ā£8m kutaka kumnunua mchezaji kiungo wa kati wa Scotland anayechezea Sheffield Wednesday Barry Bannan, 28, arejee katika klabu hiyo.(Mirror)

Bora kutoka Jumatatu

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameonya Real kuwa wana uwezekano mdogo wa kumchukua Mauricio Pochettino kutoka Tottenham kuchukua mahala pake Lopetegui. (Evening Standard)

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMauricio Pochettino

Makamu wa rais wa Juventus Pavel Nedved amekana madai ya kumsaini tena kiungo wa kati wa Manchester United mfaransa Paul Pogba, 25. (Sky Italia, kupitia Inside Futbol)

Jedwali La Msimamo Wa Ligi Ya Epl 2018/19


Manchester United na Chelsea wanatarajiwa kushindania kumsaini kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 27. (Express)

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionAaron Ramsey

Kiungo wa kati wa Chelsea raia wa Croatia Mateo Kovacic, 24, aliyekuwa kwenye mkopo kutoka Real Madrid anasema ni mapema sana kuzungumzia kuhama kabisa lakini anasema anafurahishwa sana na maisha ya London. (Evening Standard)



Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 21, hajawahi kufurahia kuwa mchezaji wa ziada hata wakati alikuwa na umri wa miaka mitano, kwa mujibu wa kocha wake wa zamani. (Mirror)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...