Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CCM

Maalim Seif kutimkia ACT-Wazalendo

Chama cha Wananchi (CUF) upande wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba umedai Maalim Seif Sharif Hamad anajiandaa kuhamia ACT-Wazalendo. Zitto Kabwe akiwa na Maalim Seif pamoja na Edward Lowassa. Amesema Maalim Seif ambaye ni katibu mkuu wa chama hicho kwa sasa yuko mbioni kutimkia ACT. Akizungumza leo Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amedai vyama sita vya upinzani vilivyokutaka Zanzibar wiki iliyopita moja ya ajenda yao ilikuwa namna gani Maalim Seif atakubaliana na ACT-Wazalendo. Amesema miongoni mwa makubaliano hayo ni kuwa upande wa Maalim Seif uachiwe nafasi zote za uongozi upande wa Zanzibar na Zitto Kabwe ambaye ni kiongozi wa ACT, wachukue uongozi wa Tanzania Bara. Amedai kuwa hata kama Maalim Seif ataondoka CUF, wataendelea kuwa imara huku akiwataka wote watakaoambatana na katibu mkuu huyo kwenda ACT kutosita kwa s...

Mizengo Pinda azungumzia Upinzani

Mizengo Pinda azungumzia maumivu ya Upinzani Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ameweka wazi jinsi alivyokuwa akiumizwa na kauli za upinzani dhidi ya uongozi wake na kusema kuwa anaushangaa upinzani kulalamikia uongozi ambao waliulilia kwa muda mrefu. Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda. Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma, Pinda amesema kuna kipindi wakati wa uongozi wake, wapinzani walikuwa wakiinyooshea kidole serikali yao kuwa ni dhaifu haina makali, hivyo walikuwa wanataka kiongozi mkali na mwenye uamuzi mgumu. " Kauli hiyo na ilikuwa ikinikera kwa sababu ilitulenga viongozi wa wakati ule, lakini sasa nashangaa kuona wapinzani haohao wameanza kulalamika tena juu ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli ambaye ndiye kiongozi wa aina waliyekuwa wakitamani kumpata" , amesema Pinda. Pinda amesema kuwa, Rais Magufuli ndiye kiongozi ambaye Watanzania walikuwa wanamhitaji kutokana na uthubutu alionao katika kutekeleza miradi ...

MWENYEKITI WA CCM KUONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kuongoza kikao cha halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi kitakachofanyika Jijini Dar es salaam ambacho kitalenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya kisiasa nchini. Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kikiongozwa na Mwenyekiti wake Rais John Magufuli. Jana jioni Desemba 17, Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi aliongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho ambacho kilifanyika Jijini Dar es salaam, ambapo kabla ya kikao hicho, kilitanguliwa na kikao cha kamati ya usalama ya maadili. Hivi karibuni kuliibuka mvutano wa maneno baina ya Katibu Mkuu wa CCM na Dkt Bashiru Ally na moja ya Kada mkongwe wa chama hicho Bernard Membe ambaye alitajwa kupanga njama za kumuhujumu Mwenyekiti wake Rais Magufuli hali ambayo ilimfanya Dkt Bashiru kumuita kada huyo. Membe ni mmoja ya wanaotajwa kuwa huenda akawa ni miongoni mwa watakaojadiliwa kwenye vikao hivyo kutokana na mwenendo wake wa kisias...

Vyama 15 vya upinzani vyaungana

Vyama vya upinzani 15 nchini vimeungana kupinga muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ambao ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni mwezi uliopita wakati wa mkutano wa 13 wa Bunge. Baadhi ya viongozi wa vyama vilivyoshiriki kutoa tamko la pamoja Vyama vilivyoshiriki katika kutoa tamko la pamoja kupinga muswada huo ni CHADEMA, CUF, DP, ACT Wazalendo, NLD, ADC, CCK, UPDP, Chauma, NCCR Mageuzi vikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chauma), Hashim Rungwe. Akisoma tamko la pamoja katika mkutano huo, Mwenyekiti wa muungano huo, Hashim Rungwe amesema kuwa wameamua kuichagua siku ya leo ya Uhuru kwakuwa ni siku muhimu ya kukumbukwa kwa nchi japokuwa haijasheherekewa kama ilivyozoeleka. " Tumeitumia siku ya leo ya Uhuru kutoa tamko hili kwani ni siku muhimu kwa taifa letu na serikali ya awamu ya tano kuendelea kufuta sherehe za Uhuru ambazo Duniani kote ni siku ambayo taifa husheherekea kuzaliwa kwake , " amesema. Kuhusu msimamo wa umoja huo kwenye sheria ...

Chadema watoa taarifa kuhusu Jeshi la Polisi kumshikilia dereva wa Mbowe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelalamikia hatua ya  Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumshikilia kwa siku mbili  mtumishi wao Williard Urassa.  Urassa ambaye ni dereva wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikamatwa jana nje ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.  Taarifa iliyotolewa leo, Novemba 24, 2018 na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imeeleza tangu Urassa alipokamatwa na polisi, jeshi hilo limekataa kumpatia dhamana huku likizuia mtu yeyote kuonana naye.  Hii ndio Taarifa kamili:   Kwa siku ya pili leo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Ndugu Williard Urassa, ambaye ni mtumishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Makao Makuu, bila kueleza sababu za kumshikilia, huku pia akinyimwa haki zake za msingi, kinyume cha sheria za nchi.  Ndugu Urassa ambaye ni Dereva wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, alikamatwa jana nje ya chumba cha Mahakama y...

Zitto alilia rushwa

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amefunguka kuwa suala la rushwa limepigiwa kelele sana na vyama vya upinzani nchini, hivyo basi chama tawala kilitazame hilo kupitia vikao vyake vya ndani.  Zitto amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa 'twitter' ambapo ameandika kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally azungumzie mambo yanayoendelea nchini katika vikao vya ndani na asiishie kuzungumza kwenye majukwaa ya nje pekee.  “Upinzani umelalamika sana suala la rushwa kwenye uchaguzi, tuangalie hili suala la chaguzi za marudio. Wananchi wamechoshwa na siasa za hamahama ya wabunge na madiwani, hilo nalo mwalimu Bashiru alizungumzie kwenye vikao vya CCM”, ameandika Zitto.  Ameongeza kuwa ,“Siasa za nyimbo za mbele kwa mbele ni za CCM, sasa ni vyema mwalimu Bashiru akaeleza hayo katika vikao vya kamati Kuu na Halmashauri kuu ya chama chake, asiishe kwenye MVIWATA”....

Kinana amkabidhi Bashiru kijiti CCM

Enzi mpya imeanza katika chama tawala nchini Tanzania CCM baada ya msomi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk Bashiru Ally kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Abdulrahman Kinana siku ya Alhamis(31.05.2018). Msomi  huyo aliyesifika kutokana na uchambuzi wa masuala ya siasa na kupenda kushiriki mijadala ya majukwaani sasa ameingia kwenye ulingo halisi wa kisiasa na anatazamiwa kuanza kukabiliana na hoja kutoka upinzani ambao wakati fulani alikaa nao meza moja kupigania yale yanayoonekana kuwa ni masuala ya pamoja ya kitaifa. Ujio wake ndani ya CCM tayari umezusha mjadala wa hoja hasa kutokana na misimamo yake aliyokuwa akiionyesha wakati alipokuwa akishiriki kwenye mijadala ya wazi ikiwamo ile iliyohusu hali ya kisiasa nchini na umuhimu wa kuwa na katiba mpya. Katibu mkuu mpya wa CCM Dr. Bashiru Ally aliyekuwa mhadhiri UDSM Katika moja ya mijadala hiyo, msomi huyo ambaye anatajwa kuwa ni mtu mwenye kuegemea falsafa za kijamaa na uzalendo, aligusia kwa ...

"Mimi sina jipya"- Dkt. Bashiru

Katibu mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, ameeleza dhamira yake ya kusimamia misingi ya waasisi wa chama hicho ikiwemo azimio la Arusha pamoja na Katiba ya Chama hicho kikongwe nchini Tanzania. Akizungumza kwa njia ya simu kwenye kipindi cha East Africa BreakFast kinachorushwa na East Africa Radio, Dkt. Bashiru amefunguka dhamira yake ya kukiimarisha chama kwa kutetea wanyonge na kujenga imani kwa wanachama na watanzania wote. “Nafasi hii nimepewa ikiwa imeshakaliwa na watu wakubwa, nampongeza sana rafiki yangu Abdulrahman   Kinana, kwa kukiacha chama kikiwa madarakani.  Natarajia kwamba ataendelea kutoa mchango wake wa ushauri, akiwa na wenzake wengine waliostaafu katika utumishi wa chama, upande wa hadhi yangu mimi sina jipya, tunalo azimio la Arusha, tunayo itikadi ya ujamaa na kujitegemea, tunayo katiba ya chama, tunayo katiba ya nchi, hiyo ndiyo miongozo yetu kwahiyo mie sina jipya, mbali nakuwaahidi utumishi, utumishi ulio katik...

CCM yatoa ufafanuzi juu ya kujiuzulu kwa Kinana

Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey PolePole amefunguka na kudai hajapokea taarifa zozote za kujiuzulu Katibu mkuu Taifa wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kama zinavyoenezwa katika mitandao ya kijamii. Polepole amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na eatv.tv alasiri ya leo Mei 27, 2018 baada ya kuenea uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa ndg. Abdulrahman Kinana ameandika barua rasmi ya kujiuzuli nyadhfa zake anazozishikilia ndani ya CCM. "Taarifa kama hiyo huwa haitokagi kienyeji bali hutoka nje baada ya vikao kufanyika. Mimi ni mtu mdogo kwenye chama cha Mapinduzi kuelewa jambo kama hilo nje ya vikao. Ninachojua mimi Katibu Mkuu hajaniambia habari yoyote kuhusu kujiuzulu",  amesema Polepole Msikilize hapa chini Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey PolePole akitoa ufafanuzi kamili juu ya tukio hilo

Uingereza yawatahadharisha raia wake wanaoelekea Tanzania Aprili 26

Bendera ya Uingereza Iwapo wewe ni raia wa Uingereza na unapanga kusafiri kuelekea Tanzania wiki hii unatakiwa kuwa mwangalifu ili kuhakikisha kuwa haujipati katika maandamano ya kisiasa yanayopangwa kufanyika tarehe 26 Aprili . Katika tahadhari ya usafiri iliotolewa na ubalozi wa Uingereza, wasafiri wameonywa kwamba ijapokuwa safari za kuelekea taifa hilo hazina matatizo yoyote, wageni wanaoingia nchini humo siku hiyo wanafaa kuwa makini kwani iwapo kutakuwa na maandano kunaweza kuwa na 'maafa'. Kulingana na gazeti la  The Citizen Tanzania , tahadhari hiyo ilitolewa kufuatia wito wa kufanyika kwa maandano dhidi ya serikali na mwanaharakati wa mtandaoni anayeishi nchini Marekani Mange Kimambi. Anadai kwamba maandamano hayo ni ya kupinga ukandamizaji wa uhuru wa kisiasa na unyanyasaji wa haki za kibinaadamu. Barua ilioandikwa na ubalozi wa Uingereza kwa vyombo vya habari nchini Tanzania Serikali tayari imepinga madai hayo na kusema kuwa maandamano hayo yata...

JPM ANG’ARA AFRIKA

-Atwaa tuzo ya uongozi bora Afrika -Ni katika tuzo za fahari ya Afrika zilizotolewa nchini Ghana -‘Hapa Kazi Tu’ yazidi kumpaisha kimataifa Na. Ibrahim Malinda. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kuingarisha nyota na jina la Tanzania kimataifa kwa  kutwaa tuzo ya uongozi bora barani Afrika. Sambamba na Rais Magufuli, wengine waliopata tuzo hizo ni pamoja na  mwanadiplomasia maarufu kutoka  Ethiopia na mke wa rais wa Ghana Rais Magufuli alishinda katika toleo la Tuzo ya fahari ya Afrika  2017/18 katika kipengele cha  Ubora katika Uongozi ambapo taarifa ya  kushinda kwa viongozi hao  imetolewa katika sherehe ya tuzo ya usiku ya Gala iliyofanyika Jumamosi 14 Aprili, 2018 katika Hoteli ya AH ya Accra, 43 Crescent Kinshasa, East Legon. Makundi mengine yalijumuisha mafanikio katika muziki, vyombo vya habari vya filamu, teknolojia na sekta za biashara ...

Magufuli aunda tume kuchunguza mali za CCM

MTEULE THE BEST Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli leo Disemba 20, 2017 ameunda tume ya watu 9 ambao watakuwa na jukumu la kufuatilia na kuhakiki mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kote nchini katika wajumbe hao yupo Wakili Albert Msando Magufuli amesema hayo leo kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kikao chake cha kwanza ambacho kimefanyika mjini Dodoma. Aidha Magufuli amewataka watu ambao wanashikilia mali za chama hicho wajitokeze na kutoa ushirikiano kwa watu hao huku akiwasisitiza wanachama wa CCM nao kutoa ushirikiano ili mali zao zisipotee. 

Sababu ya CCM kuendelea kuongoza Tanzania

MTEULE THE BEST Wakati CCM ikizidi kuimarika, vyama vingi vilivyoanzishwa katika miaka ya 1950 na 60 vilishatimuliwa madarakani, vikiwemo MCP Malawi na KANU nchini Kenya. Njonjo Mfaume Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa Shughuli ya kusukwa upya kwa safu ya uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania itahitimishwa wiki hii katika mkutano mkuu unaofanyika mjini Dodoma, katikati mwa nchi hiyo. Huu ni uchaguzi wa kwanza tangu Rais John Magufuli aliporithi uenyekiti kutoka kwa mtangulizi wake, Jakaya Kikwete. CCM inaendeleza mikakati ya kurejesha hadhi yake baada ya ushindi uchaguzi wa mwaka 2015. Licha ya kushinda urais kwa taabu, wapinzani chini ya mwamvuli wa UKAWA walipata karibu theluthi moja ya viti vyote vya ubunge na kudhibiti halmashauri katika miji muhimu ikiwemo Dar es Salaam, hii ikiwa ni rekodi mpya. Miaka miwili ndani ya utawala wa Rais Magufuli, upepo unaonekana kugeuka. Upinzani unaelekea kudhoofika, wakati CCM ikiimarika na kung'ara m...

MAGUFULI: MJUE MNA MIAKA MITANO YA KUUMIA TENA

MTEULE THE BEST Mwenyekiti wa (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wajumbe wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kuwa endapo watachagua viongozi kama waliokuwepo awali watambue watapata shida kwa miaka mingine mitano. Magufuli amesema hayo leo Disemba 10, 2017 akiwa Makao Makauu ya nchi mjini Dodoma alipohudhuria Mkutano Mkuu wa tisa wa UVCCM Taifa ambapo amewataka vijana wa chama hicho wasiogope kufanya maamuzi yenye kuleta mabadiliko katika safu ya uongozi wa Umoja huo kwa kuwa viongozi waliokuwepo tayari wameonyesha kuwa na dosari na kuwakosesha nafasi vijana wengi kuweza kupewa nafasi katika serikali ya awamu ya tano. "Mwenyekiti mtakaye mchagua, Makamu Mwenyekiti na uongozi wote wa vijana mtakaouchagua leo hao ndiyo watakuwa washauri wangu wakubwa ila mkichagua kama wale ambao hawakunishauri hata kwa kuniletea majina ya kuteua kwenye nafasi zenu, mkachagua tena katika mwaka huu mjue mna miaka mitano mingine ya kuumia"  alisisitiza Rais Magufuli  Aidha R...

HUMPHREY POLEPOLE LEO KWENYE PRESS CONFERENCE.*

*NUKUU ZA NDG. HUMPHREY POLEPOLE LEO KWENYE PRESS CONFERENCE.* Tarehe 27/11/2017. "Chama Cha Mapinduzi tulikaa na tulifanya mafunzo kwa watumishi wetu wote kwenye ngazi na maeneo ambazo tunafanya uchaguzi" Ndg  Humphrey Polepole. "Wagombea wetu pahala pote walijinasibu kuuza na kufafanua ilani ya uchaguzi". Ndg. Humphrey Polepole "Kwa vyama vya siasa, Ukiona hoja zako zinafanyiwa kazi na serikali unatakiwa kufurahi na siyo kuhujumu" Ndg. Humphrey Polepole. "Wagombea wote wa Chama Cha  Mapinduzi waliimba ilani ilani". Ndg. Humphrey Polepole "Wanachama wa Chama cha Mapinduzi walishiriki kujipanga" Ndg. Humphrey Polepole "Chama kikaelekeza mikoa yenye uchaguzi kufanya siasa ya kisayansi siasa inayoshughulisha na shida za watu" Ndg. Humphrey Polepole "Kampeni hizi kimsingi zimefanyiwa kazi na viongozi wa Mikoa wa Chama Cha Mapinduzi" Ndg. Humphrey Polepole. "Katika siku mbili za mwisho tulipeleka vio...