BALOZI DKT. NCHIMBI AZUNGUMZA NA DKT. MPANGO

BALOZI DKT. NCHIMBI AZUNGUMZA NA DKT. MPANGO


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi alizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdory Mpango, baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa. 


Mkutano huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ulifanyika kwa njia ya mtandao katika Ukumbi wa Mikutano wa NEC, Makao Makuu ya CCM, Jumamosi tarehe 26 Julai 2025, jijini Dodoma.


Aidha, wanaoonekana katika picha ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, ambao ni, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko (kulia) pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe Zubeir Ali Maulid. 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU