Umati mkubwa wahudhuria kuapishwa kwa Mnangagwa Emmerson Mnangagwa ameapishwa kama rais mpya wa Zimbabwe , huku kukiwa na miito ya kumtaka amalize "utamaduni wa ufisadi''. Emmerson Mnangagwa ameapishwa rasmi baada ya kurejea nyumbani kutoka uhamishoni Jumatano Raia wa Zimbabwe wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa michezo mjini katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa. Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla. Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ameapishwa katika uwanja michezo wa Harare. Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke . Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi". Taarifa ya kuondoka mada...