Mwanajeshi wa Korea Kaskazini aliyepigwa risasi 6 apata afueni





Mwanajeshi wa Korea Kaskazni akikimbizwa hospitali baada ya kupigwa risasi sita na wanajeshi wa taifa lake alipokuwa akitoroka





Mwanajeshi mmoja wa Korea Kaskazini ambaye alipigwa risasi 6 alipokuwa akivuka mpaka wa nchi hiyo, katika harakati za kutoroka, amepata afueni na sasa anaweza kuwasiliana na wahudumu wa kimatibabu.





Madaktari wanasema kuwa wamemtaka atizame runinga na kwa sasa anaonyeshwa filamu za Korea Kaskazini.





Wiki iliyopita, askari huyo aliamua kulitoroka taifa hilo, kwa ujasiri mkubwa, ili kuingia kwenye ardhi ya taifa jirani la Korea Kusini, hatua iliyowalazimu wanajeshi wenzake kummiminia zaidi ya risasi 40, huku sita zikimpata.





Wengi walidhani amefariki, lakini kwa kudra za mwenyezi Mungu, yungali hai.





Wafanyikazi katika Hospitali hiyo wanasema kuwa japo askari huyo anahuzuni nyingi, wamemwekea bendera ya Korea Kaskazini ukutani karibu na kitanda chake, ili kumliwaza




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU