Magereza ya Ujerumani yanajitahidi kukabiliana na wafungwa wenye itikadi kali Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka baada kufunguliwa kwa misururu ya uchunguzi unaohusiana na ugaidi katika miezi ya hivi karibuni. Takriban Waislamu 150 wenye itikadi kali wanashikiliwa katika magereza ya Ujerumani, kwa mujibu wa takwimu za afisi ya Idara ya Upelelezi ya Serikali kuu ya Ujerumani zilizoschapishwa kwenye gazeti la kila siku nchini Ujerumani la Die Welt. Gazeti hilo lililonukuu afisi ya Idara ya Upelelezi ya Serikali Kuu, linasema kuwa wanaume hao ama wanatumikia kifungo au wanatuhumiwa kwa makosa yanayohusiana na ugaidi. wafungwa wanaishikiliwa walikuwa wapiganaji wa IS Wapiganaji wa Dola la Kiislamu-IS Gazeti hilo linaendelea kusema kuwa, watu kadhaa wanaohusishwa na ugaidi wanashikiliwa katika magereza hayo ambao huenda ni wafuasi wanawaunga mkono itakadi kali. Waziri wa sheria wa jimbo la Hesse nchini Ujerumani Eve Kuöhene-Hö ameliambia gazeti hilo kuwa, katika m...