MTEULE THE BEST Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa wito wa kutafakari upya mtazamo wa serikali ya Ujerumani kuelekea Uturuki baada ya nchi hiyo kuwakamata raia wawili zaidi wa Ujerumani. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeporomoka tangu jaribio lililoshindwa la mapinduzi mwaka 2016. Hakuna "msingi wa kisheria" wa kukamatwa katika matukio mengi, Merkel amesema , akielezea kuhusu Wajerumani wawili waliokamatwa siku ya Alhamis nchini Uturuki, na kufikisha jumla ya idadi ya raia wa Ujerumani waliokamatwa nchini humo kwa sababu za kisiasa kuwa 12. "Hii ndio sababu tunahitaji kuchukua hatua muhimu hapa," amesema , na kuongeza kwamba serikali "huenda inapaswa kutafakari upya" uhus...