Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mahujaji waanza ibada ya Hajji mjini Makka

MTEULE THE BEST

Zaidi ya Mahujaji milioni mbili wa Kiislamu kutoka duniani kote leo Jumatano wanaanza ibada ya Hajji katika maeneo matakatifu ya Makka na Madina ikiwa ni nguzo kuu kwa kila muislamu kuitimiza katika maisha yake.
Hii ni moja ya nguzo kuu za kidini ambayo kila Muislamu anapaswa kuitekeza angalau mara moja katika maisha yake ikiwa anao uwezo wa kufanya hivyo. Mwanzoni mwa Hajji leo, mahujaji walianza kwa kuzunguka nyumba ya mwenyezi Mungu ya Kaaba mjini Makka na kutekeleza ibada zinazoaminika kufuatilia nyayo za Mitume Ibrahim na Ismail.
Zaidi ya mahujaji milioni mbili wanashiriki ibadi hii kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mamla za Saudia, idadi hii ikiwa ni zaidi ya waliohudhuria Hajji ya mwaka jana waliokadiriwa kufika milioni 1.8 na elfu 24,000 mwaka 1941. Afisa mmoja wa Indonesia ameliambia gazeti la Saudia kwamba jumla ya Mahujaji 221,000 kutoka Indonesia tayari wamefika mjini Makka ikiwa ndiyo idadi kubwa kutoka nje ya nchi.
Haddsch Islamische Pilgerfahrt nach Mekka | Kabaa, GroƟe Moschee (picture-alliance/AP Photo/K. Hamra)
Mahujaji mjini Makka wakigusa nyumba ya mwenyezi Mungu Kaaba
Hali ya usalama 
Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia inasema imesambaza maafisa wa usalama zaidi ya 100,000 ili kuhakikisha usalama. Walinzi wengine wa kiraia elfu 17,000 wakisaidiwa na magari karibu 3000 wanasaidia kulinda usalama. Msemaji wa wizara hiyo Meja Jenerali Mansour Al-Turki amesema, "kwa kawaida tunakuwa na idadi ile ile ya vikosi vya usalama wakati wa Hajji na idadi inaongezeka na kupita 100,000, wanachama wamegawanyika katika majukumu tofauti ili kulinda usalama. Kwa kila afisa usalama ana majukumu mawili, Moja ni kumlinda hujaji na pili ni mpango unaohusiana na kila mtu anachopaswa kuetekeleza katika eneo hili."
Pamoja na hilo, Saudi Arabia imeweka maelfu ya kamera za usalama katika njia watakazopita mahujaji huku maelfu ya mabanda yaliyo na viyoyozi yakiwekwa katika eneo la Mina kati ya mlima Arafat na Makka ili kuwahifadhi mahujaji. Shirika la Hilali nyekundi la Saudia pia limeongeza wafanyakazi wa ziada 2,468 pamoja na wale wa kujitolea takribani 500 ambao watafanya kazi na magari 326 ya kubebea wagonjwa na helikopta nane.
Saudi Arabien | Muslimische GlƤubige beten in der PilgerstƤtte Mekka (picture-alliance/AP)
Mahujaji wa Kiislamu wakiswali katika msikiti mkuu kabla ya kuanza kwa Hajji
Kwa mujibu wa taarifa za habari za nchini humo zaidi ya wapishi 700 wameajiriwa ili kuwahudumia waumini hao. Saudi Arabia ina matumaini ya kuwakaribisha mahujaji milioni 30 kwa mwaka hadi kufikia 2030 katika ibada mbalimbali za Hajji. Mmoja wa Mahujaji kutoka Misri Ahmed Ali anasema, "asanteni nyote, kama mnavyojua ni hisia zisizoelezeka, ni Hajji yangu ya kwanza na namshukuru Allah. Kila kitu kiko sawa. haielezeki, ni hisia za kiroho. Asante Allah najisikia vizuri."
Mgogoro wa kidiplomasia
Hajji ya mwaka huu inashuhudia mahujaji wa Kishia kutoka Iran wakirejea kufuatia mgogoro wa  kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Kiislamu na hasimu wake wa Kisunni Saudi Arabia. Pia inakuja wakati ukanda wa Ghuba ukigubikwa na mgogoro wa kisiasa na makundi ya wanajihadi wa Kiislamu wakikabiliwa na mbinyo nchini Syria na Iraq.
Mamlaka za Saudi Arabia zimewekeza pakubwa kuhakikisha kwamba mauaji ya 2015 yaliyopelekea watu karibu 2300 kupoteza maisha wakiwemo Wairan 464, hayajirudii.
Riyadh na Tehran zilikata mahusiano miezi michache baadae, baada ya hukumu ya kifo dhidi ya mhubiri wa kishia nchini Saudi Arabia na kuchochea mashambulizi katika balozi za Saudi nchini Iran.
Hajji hiyo pia inaanza katikati mwa mgogoro wa kidilpmasia kati ya mataifa kadhaa ya kiarabu na Qatar inayotuhumiwa kwa kuyafadhili makundi yenye itikadi kali na kwa kuwa karibu na mpinzani mkuu wa Riyadh yani Tehran.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...