MTEULE THE BEST
Arsenal wanafanya jaribio la dakika za mwisho kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain Julian Draxler, 23, na wakimkosa watazuia uhamisho wa Alexis Sanchez, 28, kwenda Manchester City. (Daily Mirror)
Manchester City watapanda dau la pauni milioni 70 taslimu kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, na tayari wamepeleka kikosi chake cha wansheria na madaktari nchini Chile kwa ajili ya kukamilisha usajili huo. (Independent)
Matumaini ya Manchester City ya kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29, bado ni ati ati, kwa sababu Eliaquim Mangala, 26, ambaye angehusika katika mkataba huo hataki kwenda West Brom.
- Oxlade Chamberlain aikataa Chelsea, ataka kwenda Liverpool
- Liverpool kumsajili Oxlade Chamberlain kwa £40m
Arsenal na Leicester walipanda dau la pauni milioni 25 kumtaka beki huyo, lakini maombi yao yalikataliwa. (Daily Telegraph)
Crystal palace wana matumaini ya kumsajili Eliaquim Mangala kutoka City kwa pauni milioni 23. (Sun)
Swansea wanakaribia kumsajili kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches kwa mkopo. (Guardian)
West Ham wanapanga kumchukua Jack Wilshere, 25, kwa mkopo kutoka Arsenal. (Sun)
Baada ya kukosa mtu wa kumsaidia Victor Moses, Chelsea wanafikiria kumsajili Bacary Sagna. (Daily Star)
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, anakaribia kujiunga tena na Atletico Madrid ambao wametoa dau jipya la pauni milioni 49 ambazo Chelsea wanafikiria kuzipokea. (Sun)
Chelsea bado wapo kwenye mazungumzo na Everton ya kumsajili kiungo mshambuliaji Ross Barkley, 23, huku muda ukizidi kutaradad wa kusajili wachezaji watatu wapya ambao Antonio Conte aliwataka. (Daily Telegraph)
Tottenham pia wanafikiria kumsajili Ross Barkley. (Evening Standard)
Tottenham wanaongoza katika mbio za kutaka kumsajili winga wa Leicester City Demarai Gray kabla ya dirisha la usajili kufungwa leo. (Daily Mirror)
Tottenham wanajiandaa kukamilisha usajili wa beki wa kulia wa PSG Serge Aurier, 24, kwa pauni milioni 23 baada ya wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza kumpa kibali cha kufanya kazi. (Guardian)
Barcelona, Chelsea na Tottenham zinamnyatia winga wa Leicester City Riyad Mahrez, 26. (L'Equipe)
Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya kina na Swansea ya kumsajili mshambuliaji Fernando Llorente, 32. (ESPN)
Everton wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Mitchy Batshuayi. (FootMercato)
Liverpool wanaendeleza juhudi zao za kumsajili kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21, na wamepanda dau la pauni milioni 74. (Independent)
Liverpool tayari wameandaa madaktari kusafiri kwenda Paris kwa ajili ya vipimo vya afya vya Thomas Lemar, wa Monaco, iwapo makubaliano yatafikiwa baina ya timu hizo mbili. (Liverpool Echo)
Liverpool pia wapo tayari kutoa pauni milioni 75 kumsajili beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk, 26, ingawa Southampton wamesema hawataki kumuuza. (Times)
Meneja wa Newcastle anataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, kuziba nafasi ya Dwight Gayle ambaye anataka kuondoka. (Express)
Fulham wamepanda dau la pauni milioni 15 kumtaka mshambuliaji wa Newcastle Dwight Gayle, 27, lakini Newcastle wanataka pauni milioni 18-20. (Daily Mail)
Newcastle wanatarajiwa kuwa na pilikapilika nyingi leo kabla ya dirisha la usajili kufungwa huku wakitaka kumsajili kwa mkopo winga wa Chelsea Kenedy, 21. (Evening Chronicle)
Tottenham na West Ham wapo tayari kupambana kumsajili kiungo wa Barcelona Andre Gomes, 24. (Daily Mirror)
Everton wamepanda dau kumtaka beki wa Barcelona Thomas Vermaelen, 31, kwa mkopo. (Liverpool Echo)
**Dirisha la usajili Uingereza lafungwa leo saa saba usiku saa za Afrika Mashariki
Maoni