Polisi Rwanda wafanya msako nyumba ya aliyetaka kuwania urais

MTEULE THE BEST
Diane Shima Rwigara
Image captionDiane Shima Rwigara alizuiwa kuwania urais
Polisi nchini Rwanda wamekanusha kwamba wanamzuilia mwanamke aliyetaka kuwania urais katika uchaguzi uliofanyika mapema mwaka huu.
Taarifa zilikuwa zimeenea mitandao ya kijamii nchini humo kwamba polisi wamemkamata Diane Shima Rwigara na mamake.
Msemaji wa Polisi ya Rwanda Theos Badege ameiambia BBC kuwa polisi walifanya upekuzi nyumbani kwake kama sehemu ya upelelezi wa mwanzo kuhusu makosa anayotuhumiwa yeye na familia yake ambayo ni pamoja na kosa la kughushi nyaraka na kukwepa kulipa kodi.
Taarifa zilikuwa zimesema kuwa watu wasiojulikana ambao walikuwa na silaha lakini walivalia mavazi ya kiraia walivamia nyumbani kwa mwanasiasa huyo mapema leo Jumatano.
Familia yake inasema kufikia sasa bado mwanamke huyo na mamake hawajulikani waliko.
Diane Rwigara alikataliwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu ambapo Rais Paul Kagame alishinda kwa kura nyingi.
Mwanasiasa huyo, ambaye amekuwa akitetea haki za wanawake nchini humo, baadaye alianzisha kundi la kukosoa utawala wa nchi hiyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU