Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya VITA

Bob Junior: Simba aliyekuwa 'mfalme' wa Serengeti auawa na wapinzani

Bob ametawala eneo lake kwa miaka saba Simba anayejulikana kwani mfalme wa Serengeti ameuawa na wapinzani.  Waendeshaji watalii na wageni katika mbuga ya kitaifa wametoa pongezi kwa "mwisho" Bob Junior - anayejulikana pia kama Snyggve - mtandaoni. "Paka aliyepiga picha" na "paka baridi zaidi" huko Serengeti, Bob Jr alikuwa na sifa ya kutisha kati ya wapinzani wake na alikuwa ametawala kwa miaka saba kwa msaada wa kaka yake, Tryggve. Wapinzani wadogo wanaaminika kuwaua wawili hao.  "Walitaka kumpindua Bob Junior," afisa wa hifadhi ya Serengeti Fredy Shirima aliambia BBC.  "Matukio haya kwa kawaida hutokea wakati mkuu wa kiburi anazeeka au wakati mwingine wakati simba wengine hawafurahii udhibiti wake juu ya eneo kubwa," aliongeza. "Inafikiriwa kaka yake pia alikumbana na hali hiyo hiyo, lakini tunajaribu kuthibitisha hili," Bw Shirima alisema, akiongeza kuwa wawili hao waliuawa katika mashambulizi tofauti lakini yak...

Mashambulio ya angani yakwamisha amani Israel na Gaza

Gaza imeshuhudia mashambulizi zaidi ya angani baada ya roketi kuelekezwa Israel Israel imefanya mashambulio mapya ya angani dhidi ya ngome ya wanamgambo baada ya roketi iloyorushwa kutoka Gaza kuanguka katika eneo lake, hatua ambayo huenda ikalemaza juhudi za kusitisha mapigano. Vyombo vya habari vya Palestina vinasema makombora ya Israel yalilenga maeneo yanayokaliwa na kundi la Kipalestina la Islamic Jihad (PIJ) mapema siku ya Ijumaa, na kuwajeruhi. Hii ni baada ya roketi tano kurushwa katika ardhi ya Israel Alhamisi baada ya PIJ kuitikia wito wa kusitisha mapigano. Ushawishi wa Iran 'unaongezeka' mashariki ya kati Mapigano yalizuka baada ya Israel kumuua kamanda wa PIJ siku ya Jumatatu. Israel ilisema Baha Abu al-Ata alikuwa "mtu hatari"ambaye alihusika kupanga shambulio la roketi la hivi karibuni kutoka Gaza. Zaidi ya maroketi 450 yalirushwa Israel, katika mashambulio kadhaa ya angani yaliyofanywa kutoka Gaza katika muda wa siku mbili . Mzozo kati ya Isr...

Korea Kaskazini 'yaiba mabilioni kutengeza makombora'

Korea Kaskazini inasema jaribio la hivi karibuni la makombora yake ni onyo kwa Marekani na Korea Kusini Korea Kaskazini imeiba dola bilioni mbili (£1.6bn) kufadhili mpango wake wa silaha kupitia uvamizi wa kimtando, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyovuja. Ripoti hiyo ya kisiri inasema Pyongyang inalenga mabenki na na ubadilishanaji wa sarafu ya crypto-currency kukusanya pesa. Vyanzo vya habari vimethibitishia BBC kwamba UN ilikuwa ikichunguza mashambulio 35 ya kimtandoa. Korea Kaskazini ilifyetua makombora mawili siku ya Jumanne ikiwa ni mara ya nne imechukua hatua hiyo katika kipindi cha chini ya wiki mbili Katika taarifa, Rais wa nchi hiyo Kim Jong-un amesema hatua hiyo ni onyo dhidi ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini. Pyongyang imeelezea kuwa mazoezi hayo yanakiuka mkataba wa amani. How could war with North Korea unfold? Ripoti t iliyovuja na ambayo ilitumwa kwa kamati ya vikwazo vya Korea Kaskazini katika Baraza Kuu...

Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanaitia tumbo joto Marekani na washirika wake

Marekani yajitoa katika mkataba wa nyuklia wa enzi za vita vya baridi na Urusi Rais Vladimir Putin na Donald Trump, katika picha ya mnamo 2017 Marekani inatarajiwa kujitoa rasmi katika mkataba wa nyuklia na Urusi, hatua inayozusha hofu kuhusu ushindani wa silaha mpya. Mkataba huo unaohusu zana za nyuklia za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987. Ulipiga marufuku makombora ya masafa ya kati ya kilomita 500-5,500. ' Lakini awali mwaka huu Marekani na Nato ziliishutumu Urusi kwa kukiuka makubaliano hayo kwa kufyetua aina mpya ya kombora, jambo ambalo Moscow inalikana. Marekani imesema ina ushahidi kuwa Urusi imetuma kombora aina ya 9M729 linalofahamika kwa Nato kama SSC-8. Tuhuma hizi ziliwasilishwa kwa washirika wa Nato wa Marekani ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani. Makombora mapya ya 9M729 ya Urusi yanaitia tumbo joto Marekani na washirika wake Rais Donald Trump m...

KOREA KASKAZINI YA TOA ONYO KALI KWA KOREA KUSINI

Korea Kaskazini yatoa onyo kwa Korea Kusini kwamba ni vigumu kujilinda dhidi ya kombora lake jipya Korea kaskzini ilirusha makombora yake mawili katika bahari ya Japan Korea Kaskazini imetaja majaribio ya makombora yake mapya siku ya Alhamisi kuwa onyo rasmi dhidi ya kile ilichokitaja kuwa uchokozi wa Korea Kusini. Kombora hilo la masafa mafupi lilirushwa katika bahari ya Japan , pia ikijulikana kama bahari ya magharibi kutoka Wonsan katika pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini. Kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un alisema kuwa taifa lake lililazimika kuunda silaha ili kukabiliana na tishio la moja ka moja. Amesema kuwa jaribio hilo lilishirikisha mfumo wa kiufundi wa kuelekeza makombora. Matamshi ya bwana Kim yalioripotiwa katika vyombo vya habari yanajiri baada ya Korea Kaskazini kukosoa uamuzi wa Korea Kusini na Marekani kushiriki katika zoezi la pamoja la kijeshi mwezi ujao. Korea Kaskazini imetaja zoezi hilo la kijeshi kama maandalizi ya kulivamia taifa hilo. Ijapokuwa ...

Muungano wa G7 na Umoja wa mataifa walaani mapigano mapya Libya

Vikosi tiifu kwa serikali ya Tripoli vimeripotiwa kuungana na serikali kulinda mji mkuu Mataifa yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani G7, pamoja na Umoja wa mataifa yamelaani vikali mapigano yaliozuka upya nchini Libya. Mataifa hayo yanataka pande zinazohasimiana Libya "kusitisha mara moja shughuli za kijeshi". Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa wito huo. Tripoli ni makao makuu ya serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa, na ambayo pia inaungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Vikosi vya kulinda usalama vya umoja wa mataifa katika mji huo vimekuwa katika hali ya tahadhari. Ghasia zimekumba Libya tangu utawala kiongozi wa nchi hiyo wa mda mrefu, Muammar Gaddafi kuangushwa na yeye kuuawa mwaka 2011. Nini kinachofanyika ? Kamanda Khalifa Haftar, ambaye ni kiongozi wa vikosi vya kijeshi vinavyopinga utawala wa Tripoli siku ya Alhamisi aliamuru vikosi vyake kuingia mji wa Libya. Hatua hiyo ilijiri wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Ma...

Wafadhili waichangishia fedha Congo

Wafadhili wanakutana mjini Geneva Uswisi Ijumaa katika harakati za kuchangisha dola bilioni 1.7 kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambayo inakabiliwa na mzozo. Wataalam wanasema huenda mzozo huo ukapindukia na kuwa janga kubwa. Mkutano huo unakuja wakati kukiwa na hofu kwamba  mizozo ya kikabila, ufisadi na hali mbaya ya usalama ni mambo yanayozusha hofu ya umwagikaji damu. Kwa wale walioachwa bila makao, kitisho ni cha kweli. Raia mmoja wa Congo alielezea mzozo wa kikabila katika mkoa wa Ituri kwa kusema, "ni kama wakati tulipokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe." Kulingana na makadirio ya shirika la msalaba mwekundu karibu Wacongo 70,000 wamekimbilia Uganda kwa kuuvuka mto Albert tangu Januari. Ituri ni mkoa mmoja tu kati ya mingi ambayo makundi yaliyojihami na wahalifu wanawasumbua raia. Ukosefu wa usalama umezidisha idadi ya wakimbizi wa ndani ya nchi Zaidi ya hayo kuna mzozo wa kisiasa unaozunguka suala la urais ambapo watu wengi wanamtaka rais Joseph...