Gaza imeshuhudia mashambulizi zaidi ya angani baada ya roketi kuelekezwa Israel
Israel imefanya mashambulio mapya ya angani dhidi ya ngome ya wanamgambo baada ya roketi iloyorushwa kutoka Gaza kuanguka katika eneo lake, hatua ambayo huenda ikalemaza juhudi za kusitisha mapigano.
Vyombo vya habari vya Palestina vinasema makombora ya Israel yalilenga maeneo yanayokaliwa na kundi la Kipalestina la Islamic Jihad (PIJ) mapema siku ya Ijumaa, na kuwajeruhi.
Hii ni baada ya roketi tano kurushwa katika ardhi ya Israel Alhamisi baada ya PIJ kuitikia wito wa kusitisha mapigano.Ushawishi wa Iran 'unaongezeka' mashariki ya kati
Mapigano yalizuka baada ya Israel kumuua kamanda wa PIJ siku ya Jumatatu.
Israel ilisema Baha Abu al-Ata alikuwa "mtu hatari"ambaye alihusika kupanga shambulio la roketi la hivi karibuni kutoka Gaza.
Zaidi ya maroketi 450 yalirushwa Israel, katika mashambulio kadhaa ya angani yaliyofanywa kutoka Gaza katika muda wa siku mbili .
Mzozo kati ya Israel na Gaza umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa
Mapigano hayo mapya yamesababisha vifo vya wapalestina 34 na wengine 111 kujeruhiwa, huku Waisrael 63 wakihitaji huduma ya matibabu.
Israel imesema Wapalestina 25 waliouawa ni wanamgambo, waliokuwa wakijiandaa kurusha maroketi katika eneo lake.
Palestina kwa upande wake inasema kuwa waliouawa wote ni raia kutoka familia ya Abu Malhous.
Lakini majeshi ya Israel yanasisitiza kuwa kiongozi wa familia hiyo,Rasmi Abu Malhous, alikuwa kamanda wa PIJ katika kitengo cha kurusha maroketi.
Tazama jinsi roketi iliyorushwa kutoka Gaza ilivyoanguka katika barabara kuu nchini Israel
'Tuko tayari kwa mashambulizi'
Vikosi vya ulinzi vya Israel (IDF) vimesema kuwa ndege yao ilishambulia ngome ya PIJ ambayo ilitumiwa kutengeza makombora usiku kucha, pamoja na makao makuu ya wanamgambo hao katika mji wa Khan Younis.
Ilisema kuwa vikosi hivyo vimezuilia maroketi matano yaliyorushwa kutoka Gaza tangu hatua ya kusitisha mapigano ilipotangazwa, na kutaja kuwa ukiukaji mkubwa wa mkataba ambao "ni mbaya sana".
Pande zote mbili zimeonya kuwa ziko tayari kulipiza kisasi zikishambuliwa.
IDF imesema itaendelea na ''opereseni yake hali ikilazimu" ili kulinda raia wa Israel, huku mrengo wa kijeshi wa PIJ ukisema wapiganaji wake "wako tayari kwa mashambulizi".
Israel haijawahi kushambulia maeneo yanayokaliwa na kundi kubwa la wanamgambo wa Gaza, Hamas, ambalo imekuwa ikiiwajibisha kwa mashambulio yoyote ya wanamgambo kutoka Gaza.
Wachambuzi wanasema hatua hii ya sasa inaashiria kuwa Israel inalichukulia kundi la PIJ, kama hasimu mkuu wa Hamas, ambaye anafanya mashambulio bila kujali na kwamba haiko tayari kuruhusu mzozo wa mpakani utakaoingiza Hamas katika mapigano.
Lakini Kundi la Islamic Jihad ni kina nani?
Kundi la Islamic Jihad laapa kulipiza kusasi mauaji ya Baha Abu al-Ata
Kundi la Palestina la Islamic Jihad ni moja ya makundi mawili makuu ya kigaidi ya Palestina katika eneo la ukanda wa Gaza ambalo ni dogo likilinganisha na vugu vugu la linaloongoza la Hamas.
Lakini linajivunia ungwaji mkono wa wa moja kwa moja kutoka kwa Iran, kifedha na kijeshi, hatua ambayo imeifanya kuwa kiungo muhimu katika makabiliano dhidi ya Israel.
Kunda la Hamas, ambalo lilichukuwa uongozi wa eneo la Gaza mwaka 2007 kutoka kwa mamlaka ya Palestina iliyokuwa ikitambuliwa kimataifa, mara nyingi haina uwezo wa kuchukua hatua ya kijeshi kwasababu ina jukumu la kuendesha mambo katika eneo hilo ambalo linakabiliwa na mzozo.
Islamic Jihad halina jukumu hilo, na ndio maana imejipambanua kuwa mrengo wenye ujasiri, na mara kwa kwa mara limekuwa likihujumu mamlaka ya Hamas.
Kundi hili lilibuniwa mwaka 1981 kwa lengo la kuanzisha taifa la Kiislam la Palestina katika eneo la ukingo wa magharibi, Gaza na Israel.
Limeorodheshwa kama kundi la kigaidi na Marekani, Muungano wa ulaya pamoja naserikali zingine.
Mauaji ya siku ya Jumanne ya Abu al-Ata yalikuwa ya kwanza ya ngazi ya juu yaliofanywa na Israel dhidi ya kiongozi wa Islamic Jihad tangu vita vya mwaka 2014 katika eneo la ukanda wa Gaza.
Waziri mkuu wa Israel alisema Baha Abu al-Ata alikuwa''mtu hatari''
Kama ishara kuwa hadhi ya kundi hilo inaendelea kupanda viongozi wake walifanya ziara yao kwanza mjini Cairo, mwezi uliopita na kukutana na maafisa wa kijasusi wa Misri, ambao wanahudumu kama apatanishi wa Israel.
Abu al-Ata, ambaye alikuwa kamanda wa mrengo wa kijeshi wa kundi hilo alikuwa mmoja wa wajumbe katika ziara hiyo.
Uhusiano na Iran
Iran imekuwa ikiisadia kundi la Islamic Jihad kwa kuipatia mafunzo, ushauri wa kitaalamu na fedha lakini silaha zake hutengenezwa nchini humo.
Katika miaka ya hivi karibuni iliitengenezea zana za kivita ambazo zinafikia zile zinazomilikiwa na kundi la Hamas, ikiwa ni pamoja na maroketi ya masafa marefu ambayo yanaweza kushambulia mji wa Tel Aviv na maeneo ya kati ya Israel
Japo kundi hilo la kigaidi lina makao yake mjini Gaza, viongozi wake wako Beirut na Damascus, ambako limedumisha ushirikiano wa karibu na maafisa wa Iran.
Shambulio jingine la makombora linalodaiwa kutekelezwa na Israeli siku ya Jumanne lilimlenga Akram al-Ajouri, mmoja wa maafisa wake wa ngazi ya juu nchini Syria.
Vyombo vya habari vya Syria vimetangaza kuwa mashambulio ya angani ya Israel yalilenga nyumba ya kiongozi wa PIJ mjini Damascus
Kama mshirika wa kivita wa Iran, kundi hilo la kigaidi mjini Gaza ni kiungo muhimu katika mpango wa kimkakati wa Tehran kuisambaratisha Israel katika ngome zake, anasema Kobi Michael, mtaalamu wa masuala ya utafiti katika taasisi ya kitaifa ya mafunzo ya kiusalama, mjini Tel Aviv.
"Kulinga na wao hali ya utulivu ni kitu ambacho kitaimarisha Israel, na hicho ndicho kitu wasichotaka kuona kikifanyika."
Kujipata katika njia panda
Tangu ilipochukua hatamu ya uongozi mwaka 2007, Hamas imepigana mara tatu na Israel, mara nyingi kwa ushirikiano na wapiganaji wa kijihadi wa kiislamu.
Lakini Hamas imedumisha mkataba wa kusitisha vita uliofikiwa na Misri pamoja na mkataba wa amani uliofikiwa na Umoja wa mataifa na Israel katika miaezi ya hivi karibuni ili kuboresha hali ya maisha katika eneo hilo linalokaliwa na watu milioni mbili.
Katika miezi ya hivi karibuni wapiganaji wa kundi la Islamic Jihad wamekabiliana na Hamas kwa kurusha makombora, bila kutangaza kujihusisha na makombora hayo, ili kuinua hadhi yao nchini Palestina huku kundi la Hamas likidumisha mkataba wa amani wa kusitisha vita.
Hamas sasa inakabiliwa na kibarua kigumu cha kujidhibiti na kutojibu hatua ya Islamic Jihad dhidi ya Israel na kujiepusha na ghadhabu ya Palestina ikiamua kuichukulia hatua kundi hilo, Michael alisema.
"Hamas ikijaribu kujibu hatu aya kunda la Palestina la Islamic Jihad, Hamas moja kwa moja italaumiwa kwa kulemaza juhudi za kitaifa za kukabiliana na Israel,"alisema,
Kutokana na hali hiyo, Hamas inakabiliwa na kibarua cha kuamua kama itaendelea kuvumilia uchokozi wa Islamic Jihad kwa muda gani ā na ikiamua kujibu mashambulio ifanye hivyo kwa kiwango gani ā uchokozi ukiendelea.
Mkhaimar Abusada, profesa wa sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha al-Azhar mjini Gaza, anasema Hamas inafahamu fika kuwa "hali katika eneo la Gaza ni tete na kwamba makabiliano ya kijeshi huenda yakawa na athari mbaya zaidi
Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi. Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria. Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao. Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...
Maoni