Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CHUO

Utafiti: Matumizi ya simu husababisha kuwa wapenzi wengi

Utafiti: Matumizi ya simu yaliyokithiri husababisha kuwa wapenzi wengi miongoni mwa wanafunzi Matumizi ya simu yanasababisha wapenzi wengi? Katika utafiti wa zaidi ya watu 3,400 nchini Marekani wanaosoma shahada ya kwanza, wale waliosema wana matatizo na muda wanaotumia katika simu zao wanaripotiwa kuwa na wapenzi wengi pia. Na wanadhaniwa kuwa na msongo wa mawazo, mmoja wa watafiti amesema kuwa matokeo yautafiti yanashangaza. Watafiti kutoka chuo kikuu cha Chicago, Cambridge na chuo kikuu cha Minnesota wamefanya tafiti hii ya tabia za uraibu wa simu. Lengo la utafiti huu lilikua ni kutaka kujua hali ya afya ya akili ya wanafunzi na jinsi gani simu zina matokeo katika utendaji wao. Ili kujua matumizi yaliyopitiliza ya simu za mkononi, wanafunzi waliulizwa maswali mbalimbali ikiwemo yafuatayo; Rafiki zako na familia wanalalamika hukusu matumizi makubwa ya simu? Una matatizo yoyote darasani kutokana na matumizi ya simu? Unadhani muda unaotumia simu umeongezeka? ...

Prof: JOYCE NDALICHAKO AMESEMA AFRICA ITAENDELEZWA NA WAAFRICA WENYEWE

mteulethebest Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema wajibu wa kuiendeleza Afrika uko mikononi mwa Waafrika wenyewe huku jukumu la wadau wengine wa Maendeleo ni  kusaidia kukua kwa Maendeleo hayo. Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo Leo katika Mahafali ya Programu za ESAMI yaliyofanyika katika Makao Makuu ya ESAMI jijini Arusha ambapo amesisitiza kuwa  Waafrika wanapaswa kujisimamia wenyewe katika nyanja za Kijamii na Kiuchumi  kwa lengo la kutimiza malengo ya bara hilo. “ Ili Afrika iweze kuendelea lazima ijisimamie yenyewe katika masuala ya kijamii na kiuchumi na hii itawezekana tu kupitia   vijana ambao wameandaliwa  vyema na wakawa tayari kuhakikisha wanaliendeleza bara la Afrika kwa ujasiri bila kuhofia changamoto watakazokutana nazo,” alisisitiza Waziri Ndalichako Kiongozi huyo amesema bara la Afrika linahitaji Viongozi wenye ujasiri, ambao wapo tayari kuhakikisha Afrika inakwenda mbele kiuchumi na Kija...