mteulethebest
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema wajibu wa kuiendeleza Afrika uko mikononi mwa Waafrika wenyewe huku jukumu la wadau wengine wa Maendeleo ni kusaidia kukua kwa Maendeleo hayo.
Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo Leo katika Mahafali ya Programu za ESAMI yaliyofanyika katika Makao Makuu ya ESAMI jijini Arusha ambapo amesisitiza kuwa Waafrika wanapaswa kujisimamia wenyewe katika nyanja za Kijamii na Kiuchumi kwa lengo la kutimiza malengo ya bara hilo.
ā Ili Afrika iweze kuendelea lazima ijisimamie yenyewe katika masuala ya kijamii na kiuchumi na hii itawezekana tu kupitia vijana ambao wameandaliwa vyema na wakawa tayari kuhakikisha wanaliendeleza bara la Afrika kwa ujasiri bila kuhofia changamoto watakazokutana nazo,ā alisisitiza Waziri Ndalichako
Kiongozi huyo amesema bara la Afrika linahitaji Viongozi wenye ujasiri, ambao wapo tayari kuhakikisha Afrika inakwenda mbele kiuchumi na Kijamii.
Akizungumza katika mahafali hayo Mkurugenzi Mkuu wa ESAMI Prof. Bonard Mwape amesema wahitimu wote
wameandaliwa vyema kwenda kuleta Mabadiliko na Maendeleo katika nchi zao pamoja na kuhakikisha bara la Afrika linakuwa lenye maendeleo.
Mahafali hayo yamejumuisha zaidi ya wahitimu 360 kutoka nchi za Afrika ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Namibia, Mali, Malawi DR- Congo, Burundi, Zimbambwe na wenyeji Tanzania.
Maoni
The King ėķ¹ģ¹“ģ§ė ø Casino is the ź·øė¦¬ź³ ģ¹“ģ§ė øģ¬ģ“ķø new place where the ģŗė³“ėģ ģ¹“ģ§ė ø real money ėķ¹ģ¹“ģ§ė ø ģ¬ė”Æ gambling is legal in ford fusion titanium Florida and Pennsylvania. We love the new casino. We've got some great