Prof: JOYCE NDALICHAKO AMESEMA AFRICA ITAENDELEZWA NA WAAFRICA WENYEWE

mteulethebest


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema wajibu wa kuiendeleza Afrika uko mikononi mwa Waafrika wenyewe huku jukumu la wadau wengine wa Maendeleo ni  kusaidia kukua kwa Maendeleo hayo.


Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo Leo katika Mahafali ya Programu za ESAMI yaliyofanyika katika Makao Makuu ya ESAMI jijini Arusha ambapo amesisitiza kuwa  Waafrika wanapaswa kujisimamia wenyewe katika nyanja za Kijamii na Kiuchumi  kwa lengo la kutimiza malengo ya bara hilo.
“ Ili Afrika iweze kuendelea lazima ijisimamie yenyewe katika masuala ya kijamii na kiuchumi na hii itawezekana tu kupitia   vijana ambao wameandaliwa  vyema na wakawa tayari kuhakikisha wanaliendeleza bara la Afrika kwa ujasiri bila kuhofia changamoto watakazokutana nazo,” alisisitiza Waziri Ndalichako
Kiongozi huyo amesema bara la Afrika linahitaji Viongozi wenye ujasiri, ambao wapo tayari kuhakikisha Afrika inakwenda mbele kiuchumi na Kijamii.
Akizungumza katika mahafali hayo Mkurugenzi Mkuu wa ESAMI Prof. Bonard  Mwape amesema wahitimu wote 

wameandaliwa vyema kwenda kuleta Mabadiliko  na Maendeleo katika nchi zao pamoja na kuhakikisha  bara la Afrika linakuwa  lenye maendeleo.
Mahafali hayo yamejumuisha zaidi ya wahitimu 360 kutoka nchi za Afrika ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Namibia, Mali, Malawi DR- Congo, Burundi, Zimbambwe na wenyeji Tanzania.

Maoni

Bila jina alisema…
The King Casino: The New King & The World of Gaming
The King 더킹카지노 Casino is the 그리고 카지노사이트 new place where the 캄보디아 카지노 real money 더킹카지노 슬롯 gambling is legal in ford fusion titanium Florida and Pennsylvania. We love the new casino. We've got some great

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU