Loading...
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Ambwene Yesaya maarufu kama AY amethibitisha kumiliki mjengo wa kifahari nchini Marekani katika maeneo ya Calabasas.
Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers AY amethibitisha kwamba akili yake inafikiri mbali zaidi nay eye ni wa anga za kimataifa, naye akanunua Mjengo maeneo ya Calabasas ingawa hajataka kufafanua gharama zake.
Ni kweli nimefanikiwa kupata nyumba Calabasas na ndipo yatakuwa makazi yangu, ninamiliki nyumba mbili ikiwemo hiyo ya Marekani na moja Tanzania,na pia ninamiliki magari manne“.
Maoni