Ruka hadi kwenye maudhui makuu

List ya wasanii watakao perform fiesta DSM imetoka

Nandy amepigwa chini?




Moja ya story kubwa ni pamoja na kilele cha msimu wa fiesta kwa mwaka huu wa 2018 ambapo kilele hicho kitafanyika Leaders Club Dar es Salaam siku ya jumamosi ya November 24 ambapo siku ya leo 22, 2018 Waziri wa ladha na vibe kutoka Jamhuri ya Fiesta Kenedy the Remedy ameitaja listi ya Wasanii watakao Perform. 

Katika list hiyo ambayo wametajwa wasanii wakizazi jina la msanii Nandy halijatajwa na kuacha maswali kuwa huwenda Nandy amepigwa chini..? lakini pamoja na hilo bado inasubiriwa list nyingine ya kambi ya upinzani inayohusisha wasanii wakongwe kwenye game ya bongofleva. 

List ya wasanii watakao ā€“ perform 

1. Weusi 
2. Rostam 
3. Fid Q 
4. Wakazi 
5. Rich Mavoco 
6. The Mafik 
7. Ben pol 
8. Rosa Ree 
9. Marioo 
10. Barnaba 
11. Billnass 
12. Chege Chigunda 
13. Dogo Janja 
14. Msami 
15. WhoZu 
16. Mimi Mars 
17. Lulu Diva 
18. Zaiid 
19. Mesen Selekta 
20. Maua Sama 
21. Tid 
22. Qchief 
23. Juma Nature 
24.Jolie 
25.Benson 
26.Jay Melody 
27.Mabantu 
28.Brian Simba 
29. Amber Lulu 

Usisahau siku hiyo kutakuwa na mambo mengi ya Surprise hivyo jitaidi mtu wangu uwahi kupata ticket yako mapema kwa Kiingilio cha Elfu Kumi ukinunua kwa Tigopesa master-pass QR, na elfu kumi na tano kawaida

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...