Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 21.11.2018: Eriksen, Rashford, De Jong, Kante, Perisic, Rabiot, Hernandez
Frenkie de Jong
Manchester City watahitajika kulipa pauni milioni 75 kwa kiungo wa kati wa Ajax, Frenkie de Jong, ambaye pia anatafutwa na Barcelona. Mchezaji huyo wa miaka 21 pia anawinda na meneja wa City Pep Guardiola. (Mirror)
Real Madrid wanapanga kutumia pauni milioni 90 kumsaini mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 21, na paunia milioni 40 kwa kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 26. (Sun)
Kiungo wa kati Mfaransa N'Golo Kante, 27, yuko tayari kusaibi mkataba mpya na Chelesea wa thamani ya karibu pauni milioni 300,000 kwa wiki. (Telegraph)
N'Golo Kante
Real Madrid wanajaribu kumshawishi kiungo wa kati mhispania Brahim Diaz, 19, asiongeze mkataba wake na Manchester City. (AS)
Inter Milan wanafikitria ikiwa watamuuza wing'a raia wa Croatia Ivan Perisic, 29, kwenda Manchester United kwa paunia milioni 31. (Sun)
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23, ameiambia Barcelona kuwa atajiunga na klabu hiyo msimu ujao. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mohamed Elneny
Leicester wanafikiria samna kumsaini kiungo wa kati wa Arsenal raia wa Misri mwenye miaka 26 Mohamed Elneny, ambaye bado hajacheza mechi ya Ligi ya Premier msimu huu. (Leicester Mercury)
Klabu ya Ufaransa ya Nice inataka kumsaini kipa wa Liverpool mbelgiji Simon Mignolet mwezi Januari lakini mchezaji huyo wa miaka 30 anatarajiwa kubaki Anfield kwa msimu wote. (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa West Ham Javier Hernandez, 30, anatarajiwa kuondoka mwezi Januari huku timu ya Besiktas ikitarajiwa kumsaini mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United. (Sun)
Javier Hernandez
Mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic, 37, atajiunga na AC Milan mwezi Januari ambapo ataloipwa pauni milioni 1.7 kwa nusu msimu. (La Gazzetta dello Sport - in Italian)
Sevilla wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Uhispania Vicente Iborra, 30, kutoka Leicester. (COPE - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Everton raia wa Croatia Nikola Vlasic, 21, atabaki CSKA Moscow kwa mkopo licha ya Inter Milan na Roma kuwa nia ya kumsaini kwa mkataba wa kudumua. (ESPN)
Nikola Vlasic
West Bromwich Albion wako kwenye mazungumzo na kiungo wa kati wa miaka 18 Rekeem Harper kuhusu mkataba wa muda mrefu. (Express & Star)
Wolves walifanya mazungumzo na waakilishi na mshambuliaji raia wa Senegal Mbaye Diagne, 27, kuhusu kuhama kutoka klabu ya Uturuki ya Kasimpasa. (ESPN)
Bora Kutoka Jumanne
Kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba 25 anasema anataka kuondoka Manchester United na kurejea Juventus. (Corriere dello Sport - in Italian)
Pogba
Juventus wanajiandaa kumsaka raia wa England Marcus Rashford, 21, wakati wanaendelea kuonyesha nia ya kumsaini mshambuliaji huyo wa Manchester United. (Times - subscription needed)
Bisiktas wanasubiri mwezi Januari kumsaini mshambuliaji wa West Ham mwenye miaka 30 raia wa Mexico Javier Hernandez. (ESPN)
Arsenal pia wana mpango wa mwezi Januari kumwinda raia wa Uhispania Pablo Fornals, 22. Kiungo huyo wa kati wa Villarreal ana kipengee cha pauni milioni 17 cha kuvunja mkataba wake. (Sun)
Kiungo wa kati Mmarekani Christian Pulisic, 20, atahama Borussia Dortmund kujiunga na klabu ya Premier League lakini Chlsea na Liverpool wanasubiri msimu wa joto badala ya Januari. (Mirror)
Cahill
AC Milan watatoa ofa kwa mchezaji wa chelesea na England mwenye miaka 32 Gary Cahill mwezi Januari. (Corriere dello Sport - in Italian)
Mshambuliaji Mfaransa Olivier Giroud, 32, amesema hataondoka Chelsea akionya kuwa yuko tayari kupigania kikosi cha kwanza huko Stamford Bridge. (Mail)
Maoni