Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KOREA KUSINI

NATO inaingia Asia - Korea Kaskazini

DPRK ilikashifu mipango ya Tokyo ya kufungua ofisi ya kwanza ya mawasiliano yenye makao yake makuu Asia kwa kambi ya kijeshi inayoongozwa na Marekani. Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imedai NATO inataka kuongeza ushawishi wake barani Asia, ikitaja kuongezeka kwa "ushirikiano wa kijeshi" na Japan, ambayo ilikuwa mwenyeji wa ujumbe kutoka kwa muungano wa kijeshi mwezi uliopita kujadili njia za kuongeza ushirikiano. Katika maoni yaliyotolewa na Shirika la Habari la Serikali la Korea (KCNA) siku ya Jumatatu, afisa wa Kituo cha Utafiti cha Wizara ya Mambo ya Nje cha Japan, Kim Seol-hwa, alisema Washington inasukuma hatua kwa hatua NATO kuingia Asia kupitia ushirikiano na mataifa yenye nguvu za kikanda. "Ni siri iliyo wazi kwamba Marekani ... imekuwa ikijaribu kuunda muungano wa kijeshi kama huu katika eneo la Asia-Pasifiki," alisema, akiongeza kwamba "mapambano ya kijeshi ambayo hayajawahi kutokea kati ya Japan na NATO yanazua wasiwasi mkubwa na tahadhari....

Korea Kaskazini 'yaiba mabilioni kutengeza makombora'

Korea Kaskazini inasema jaribio la hivi karibuni la makombora yake ni onyo kwa Marekani na Korea Kusini Korea Kaskazini imeiba dola bilioni mbili (£1.6bn) kufadhili mpango wake wa silaha kupitia uvamizi wa kimtando, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyovuja. Ripoti hiyo ya kisiri inasema Pyongyang inalenga mabenki na na ubadilishanaji wa sarafu ya crypto-currency kukusanya pesa. Vyanzo vya habari vimethibitishia BBC kwamba UN ilikuwa ikichunguza mashambulio 35 ya kimtandoa. Korea Kaskazini ilifyetua makombora mawili siku ya Jumanne ikiwa ni mara ya nne imechukua hatua hiyo katika kipindi cha chini ya wiki mbili Katika taarifa, Rais wa nchi hiyo Kim Jong-un amesema hatua hiyo ni onyo dhidi ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini. Pyongyang imeelezea kuwa mazoezi hayo yanakiuka mkataba wa amani. How could war with North Korea unfold? Ripoti t iliyovuja na ambayo ilitumwa kwa kamati ya vikwazo vya Korea Kaskazini katika Baraza Kuu...

KOREA KASKAZINI YA TOA ONYO KALI KWA KOREA KUSINI

Korea Kaskazini yatoa onyo kwa Korea Kusini kwamba ni vigumu kujilinda dhidi ya kombora lake jipya Korea kaskzini ilirusha makombora yake mawili katika bahari ya Japan Korea Kaskazini imetaja majaribio ya makombora yake mapya siku ya Alhamisi kuwa onyo rasmi dhidi ya kile ilichokitaja kuwa uchokozi wa Korea Kusini. Kombora hilo la masafa mafupi lilirushwa katika bahari ya Japan , pia ikijulikana kama bahari ya magharibi kutoka Wonsan katika pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini. Kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un alisema kuwa taifa lake lililazimika kuunda silaha ili kukabiliana na tishio la moja ka moja. Amesema kuwa jaribio hilo lilishirikisha mfumo wa kiufundi wa kuelekeza makombora. Matamshi ya bwana Kim yalioripotiwa katika vyombo vya habari yanajiri baada ya Korea Kaskazini kukosoa uamuzi wa Korea Kusini na Marekani kushiriki katika zoezi la pamoja la kijeshi mwezi ujao. Korea Kaskazini imetaja zoezi hilo la kijeshi kama maandalizi ya kulivamia taifa hilo. Ijapokuwa ...

KOREA KASKAZINI YA RUSHA MAKOMBORA

Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa mafupi baharini Haijulikani iwapo Kim Jong Un alisimamia uzinduzi huo Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa mafupi baharini kulingana na mkuu wa wafanyikazi wa umma nchini Korea Kusini. Makombora hayo yalizinduliwa mapema siku ya Alhamisi , yakisafiri umbali wa kilomita 430 na kupaa angani umbali wa kilomita 50 kabla ya kuanguka katika bahari ya Japan , ambayo pia inajulikana kama bahari ya mashariki. Hatua hiyo inajiri baada ya taifa hilo kukasirishwa na mipango ya zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Marekeni na Korea Kusini linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao. Korea Kaskazini imeonya kwamba mazoezi hayo yatarudisha nyuma mazungumzo ya taifa hilo kutojihami na silaha za kinyuklia. Kombora la kwanza lilirushwa mwendo wa saa 05.34 mapema alfajiri na la pili mwendo wa 5.57 kulingana na Korea Kusini. Makombora hayo yalirushwa karibu na mji wa Wonsan. Haijulikani iwapo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un alisimamisha uzinduz...

RUSSIA NA CHINA ZAFANYA DORIA YA PAMOJA MAREKANI YALIA

Doria ya pamoja ya Urusi - China yazua tumbo joto Japan na Korea Kusini Korea Kusini ilisema kuwa ndege ya kijeshi ya Urusi aina ya A-50 ilikiuka anga yake mara mbili Urusi inasema kuwa imetekeleza doria yake ya kwanza ya pamoja na China , hatua iliyozifanya Korea Kusini na Japan kutuma ndege za kivita angani. Waziri wa ulinzi nchini Urusi amesema kuwa ndege nne aina ya bombers zikisaidiana na zile za kivita zilipiga doria katika njia ambayo hazikupangiwa kupitia katika maji ya Japan na bahari iliopo mashariki mwa China. Korea Kusini inasema kuwa ndege zake zilirusha makombora ya kutoa onyo wakati ndege za kijeshi za Urusi zilipoingia katika anga yake. Japan imelalamika kwa Urusi na Korea Kusini kwa tukio hilo. Kisa hicho kilitokea juu ya visiwa vinavyozozaniwa vya Dokdo/Takeshima ambavyo vinamilikiwa na Korea Kusini lakini Japan pia inadai kuwa vyake. Korea Kusini inasema kuwa ndege za kijeshi za Urusi na China ziliingia katika anga yake ilio na ulinzi mkali ya KADIZ ...

Mkutano wa Singapore bado utafanyika Juni

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesema kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ataondoa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea na kuhudhuria mkutano wa Singapore Juni 12 wa kukutana  na Rais wa Marekani Donald Trump. Katika mkutano wa ghafla wa Jumamosi, Moon na Kim wamekubaliana kwamba mkutano kati ya Marekani na Korea Kaskazini lazima ufanyike, kama Moon alivyosema katika mkutano wake na waandishi habari, mjini Seoul. "Mimi na mwenyekiti Kim tumekubaliana kwamba mkutano wa kilele wa Juni 12 lazima ufanyike kwa ufanisi, na jitihada yetu ya kupatikana rasi ya Korea isiyo na silaha za nyuklia, na utawala wa amani wa kudumu haipaswi kusimamishwa," amesema Moon. Rais wa Marekani Donald Trump kwa upande wake ameashiria kwamba maandalizi ya mkutano wa kilele wa Juni 12 yanaendelea, licha ya kuufuta mkutano huo wiki iliyopita. Mkutano huo kati ya viongozi wa Korea mbili ni mabadiliko ya hivi karibuni, katika wiki iliyogubikwa na misukosuko ya kidiplomasia kuhusi...

Viongozi wa Korea wafanya mkutano wa ghafla

Viongozi wa Korea wafanya mkutano wa ghafla Viongozi wa Korea Kaskazini na Kusini wamekutana eneo lenye ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huo ndio wa pili kati ya rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un. Unafanyika wakati pande hizo zinaendelea na jitihada za kuufanikisha mkutano wa kihistoria kati ya Korea Kaskazini na Kusini. Siku ya Alhamisi Rais wa Marekani Donald Trump alifuta mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 12 mwezi Juni lakini baadaye akasema kuwa unaweza kufanyika, Mazungumzo hayo yalifanyika upande wa Korea Kaskazini katika kijiji kinachojulikana kama Panmunjom. Bw Moon atatangaza matokeo ya mkutano huo siku ya Jumapili asubuhi. Mazungumzo kati ya Bw Trump na Kim ikiwa yatafanyika yatajikita zaidi katika kuondolewa silaha za nyuklia kutoka rasi ya Korea na kumaliza misukosuko

Korea Kaskazini yasema iko tayari kuzungumza na Marekani

Korea Kaskazini yasema bado ipo tayari kuzungumza na Marekani hata baada ya rais Donald Trump kuuvunja mkutano huo wa kilele kati yake na Kim Jong Un. Rais Trump alieleza hapo jana kwamba hatakutana na Kim Jong Un na sababu aliyoitoa ni kuwepo mazingira ya ghadhabu na uhasama wa wazi. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini, Kim Kye Gwan amesema nchi yake imesikitishwa na uamuzi huo wa Marekani. Mkutano huo ulionekana kama fursa ya kihistoria kwa Marekani kuweza kuishawishi Korea Kaskazini kuacha mpango wake wa silaha za nyuklia na siku ya Alhamisi, waandishi wa habari wa kimataifa walishuhudia Korea Kaskazini ilipokifunga kituo chake kikuu cha kufanyia majaribio ya nyuklia. Wakati Korea Kaskazini ilipotoa kauli kali dhidi ya makamu wa rais wa Marekani Mike Pence na mshauri wa masuala ya usalama wa Rais Trump, John Bolton, kauli hiyo ndio ilikuwa sababu ya Trump kuuvunja mkutano huo wa kilele kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Kiongoz...

Kiongozi wa Korea Kaskazini avuka mpaka na kuingia Korea Kusini

Rais w a Korea kaskazini Kim jong un na mwenzake wa Kusini Moon Jae-in Kim Jong-un amekuwa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kuingia Korea Kusini kwa kuvuka mstari wa kijeshi uliowekwa kugawanya mataifa hayo mawili tangu vita vya Korea 1953. Katika hatua ilioshangiliwa kwa mbwembwe za kila aina kiongozi wa Korea Kusini na mwenzake wa Korea Kaskazini walisalimiana kwa mikono katika mpaka huo. Bwana Kim alisema kuwa anatumai kwamba kutakuwa na mazungumzo ya kufana baada ya ufunguzi mzuri wakati mazungumzo hayo yalipoanza. Mkutano huo wa kihistoria utaangazia maswala ya silaha za kinyuklia na uwezekano wa makubaliano ya amani. Mengi yatakayozungumzwa ni mambo ambayo tayari yameafikiwa awali lakini wachanganuzi wengi bado wana wasiwasi kuhusu uaminifu wa Korea Kaskazini katika kukubalia kuacha shughuli ya utengezaji wa silaha za kinyuklia. Hatahivyo shughuli zote za taifa lote la Korea Kusini zilisimama kwa muda ambapo viongozi hao wawili walisalimiana kwa mikono katikati y...

Korea Kusini na Kaskazini zajiandaa kwa mkutano wa kilele

Korea Kusini imesitisha matangazo ya propaganda kwenye eneo la mpaka na  Korea Kaskazini, kabla ya viongozi wa nchi hizo mbili kukutana kwa mazungumzo yanayotarajiwa kujikita juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.  Licha ya kuwepo matumaini ya Korea Kaskazini kusitisha mpango wake wa kinyuklia, Rais wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa bado kuna njia ndefu ya kufikia suluhisho la mzozo wa Korea kaskazini  huku kiongozi huyo wa Marekani akijitayarisha kwa mkutano wa kihisitoria na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Korea zachukua hatua za maridhiano Kama sehemu ya ishara ya kujitayarisha kwa mazungumzo ya maridhiano kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini ambayo ni ya tatu ya aina hiyo tangu kukamalizika vita vya Korea vilivyodumu kati ya mwaka 1950 hadi 1953, Korea Kusini imezima matangazo ya propaganda yanayotangazwa kupitia vipaza sauti katika eneo la mpakani. Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un Korea Kusini ilikuwa  ikitangaza hab...

Dadake kiongozi wa Korea Kaskazini kutembelea K Kusini kwa ajili ya michezo ya Olimpiki

Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na mwanamke aliye na ushawishi mkubwa Korea Kaskazini atahudhuria michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi itakayozinduliwa Pyeongchang ,siku ya Ijumaa, mawaziri jijini Seoul wanasema. Kim Yo-jong, atakuwa ndugu wa kwanza wa karibu katika familia ya Kim atakayevuka mpaka. Korea zote mbili zitaandamana pamoja chini ya bendera moja katika sherehe za uzinduzi. Ushiriki wa Korea Kaskazini umeonekana kama kulegeza uhusiano baina ya nchi hizo mbili. Hata hivyo, Marekani na Japan wameishtumu Korea Kaskazini kwa kutumia michezo hio kama chama cha propaganda. Kim Yo-jong  ni nani ? Akiaminiwa kuzaliwa mwaka 1987, ni mtoto wa kike wa mwisho wa hayati kiongozi Kim Jong-il na ni dada yake wa tumbo moja Kim Jong-un. Anazidiwa umri na kaka yake kwa miaka minne na inasemekana kwamba wana uhusiano wa karibu sana. Anasemekana kuolewa na mwana wa Choe Ryong-hae, katibu wa chama tawala. Kim Yo-jong akiwa kwenye sherehe ya kuzindua jengo la ...

Korea Kaskazini na Korea Kusini zaanza mazungumzo

Korea Kaskazini na Korea Kusini wameanza mazungumzo ya Olimpiki Mkutano huo unaofanyika katika kijiji cha Panmunjom ambapo mazungumzo yao yanahusu uwezekano wa Korea Kaskazini kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi yatakayofanyika Korea Kusini mwezi wa pili. Waziri wa muungano wa Korea Kusini , Cho Myoung-Gyon amesema mazungumzo hayo yanajikita zaidi katika masuala ya olimpiki lakini mambo mengine pia yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na kutumia fursa hiyo kuimarisha uhusiano. "Tutahudhuria mkutano huu ili kuzungumzia suala la korea kaskazini kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi yatayofanyika korea kusini na kuimarisha uhusiano wan chi hizi mbili.Ninaelewa kuwa matarajio ya wengi juu ya mkutano huu ,kwanza ni kuhusu mawasiliano baina ya nchi hizi mbili ambayo yalisitishwa kwa muda.Tuna lengo la kufanya mashindano haya ya Olimpiki kuwa ya hatua ya kwanza ya kuboresha Amani baina ya nchi hizi mbili hivyo hii ni hatua nzuri na hatuna ...

Tunayoyafahamu kuhusu simu 'nyekundu na kijani' zilizotumika na nchi za Korea Kusini na Kaskazini

Hii ni simu inayounganisha Korea Kusini na Kaskazini katika nyumba ya uhuru Korea Kusini. Upande wa pili wa Korea Kaskazini ina simu kama hii Kila siku kwa miaka miwili, afisa wa Korea Kusini amechukua simu yenye rangi ya kijani na kumpigia afisa mwenzake upande wa pili , nje tu ya mpaka wa Korea Kaskazini. Lakini hamna aliyejibu simu hiyo. Hayo yote yakabadilika saa 9.30 ( 6.30 saa za GMT) tarehe 3 Januari 2018. Katika muda wa dakika 20,pande zote mbili walitumia laini zao wakiwa na matumaini ya kupungunza ugomvi baina ya nchi zao za Korea. Simu hiyo ipo katika kijiji cha mpaka wa Panmunjom, ambapo pamekuwa chanzo cha mawasiliano baina ya majirani hao ambao kimsingi bado wako vitani. Lakini tunafahamu nini kuhusu simu hiyo? 'Hamna Utani' Ni jambo linalokaa kama limetoka moja kwa moja katika nyakati za vita vya baridi - ni kweli. Likijengwa kwenye dawati mbalo ziliwekwa simu zenye rangi ya kijani na nyekunde pamoja na kompyuta, laini ya Kusini na Kaskazani ili...

Mwimbaji wa Korea Kusini Kim Jong-hyun kuzikwa leo

MTEULE THE BEST Image caption Kim Jong-hyun alikua mwanamuziki mashuhuri Korea Kusini Mazishi ya mwimbaji mashuhuri wa Korea Kusini Kim Jong-hyun, yanafanyika leo hii mjini Seoul. Mwanamuziki huyo ambaye pia alikua mtangazaji wa radio, mwandishi wa vitabu na mtunzi wa nyimbo, alikutwa amekufa katika tukio linalotajwa kuwa la kujiua. Umati mkubwa wa watu umekusanyika kumsindikiza katika safari yake ya mwisho, huku mwili wake ukibebwa na gari aina ya limousine nyeusi kutoka hospitalini alipohifadhiwa kwa takriban siku tatu. Image caption Picha yake iliwekwa hospital mjini Seoul Ibada ya kumuaga kifamilia ilifanyika mapema pia mjini Seoul. Mwanamuziki huyo aliyekua na miaka 27 akiimbia bendi ya Shinee,alikutwa ameanguka kutoka ghorofa moja refu la kupangisha siku ya Jumatatu.

Korea Kusini yaitaka Marekani kusitisha mazoezi ya kijeshi nchini humo

MTEULE THE BEST Image caption Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In ameitaka Marekani kuacha kwa muda mazoezi yake ya kijeshi nchini humo mpaka kumalizika kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika mapema mwakani. Anasema hii itasaidia pia kuifanya Korea Kaskazini kutotilia shaka uwepo wa wanamichezo wake kwenye michuano hiyo. Korea Kusini itakua mwenyeji wa michezo hiyo itakayofanyika katika mji wa Pyeongchang mwezi Februari ikiwa ni kilomita 80 kutoka mpaka wake na Korea Kaskazini. Mapema Canada na Marekani ziliapa kuendeleza mazoezi hayo ili kuisukuma Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa Nyuklia. Image caption Vikosi vya jeshi la Korea Kusini na Marekani vikifanya mazoezi ya kijeshi karibu na mpaka wa Korea Kaskazini Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa katika mgogoro wa muda mrefu kufuatia mpango wa matumizi ya mabomu ya Nyuklia unaofanywa na Korea Kaskazini. Michuano ya Olimpiki ya majira ya bariki inatarajiwa kuhusisha pia wanamichezo...

Picha za kombora jipya la Korea Kaskazini Hwasong-15 zinatuonyesha nini?

Hwasong -15 Korea Kaskazini imetoa picha  z a jaribio la kombora lake jipya ambalo inadai k u wa linaweza kushambulia popote pale nchini Marekani. Picha hizo zinaonyesha kiongozi wa Korea Kaskazini Ki Jong un na maafisa wengine kadha ya ngazi za juu jeshini wakisherehekea kombora la Hwasong-15 wakati likipaa. Lakini kombora hilo ni la aina gani? Kombora lenyewe ni kubwa. Wengi wameshangazwa na ukubwa wa kombora hilo. Picha hii ambayo haijulikanai ilichukuliwa lini na iliyotolewa na vyombo vya habari vya taifa inaonyesha Kim akilikagua kombora hilo. Kim akikagua Hwasong-15 Michael Duitsman, mtafiti katika kituo kimoja alisema kuwa kombora hilo ni kubwa kuliko kombora la kwanza la Hwasong-14 "ni nchi chache tu zinaweza kuunda kombora kama hilo na Korea Kaskazini imejiunga nazo." Hwasong-15 likipaa Pia linaonekana kuwa na kichwa kikubwa ikimaanisha kuwa linaweza kubeba bomu nzito la nyuklia kwenye kichwa chake vile Korea Kaskazini inadai. Korea Kaskazini: T...