Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara amesema mpango wa Serikali ni kujenga Mabweni katika Shule zote za Msingi na Sekondari, ili kuwanusuru na wanafunzi wa kike na suala la mimba. Mwanafunzi mwenye mimba Naibu Waziri Waitara ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza Bungeni jijini Dodoma leo Novemba 15, 2019 wakati wa kipindi cha maswali na majibu kutoka kwa Wabunge kwenda kwa Mawaziri. Waitara amesema kuwa " mpango wa Serikali ni kujenga Mabweni katika Shule zote za Msingi na Sekondari ili watoto wakike wapate sehemu za kukaa na tuwaepushe na mimba zitakazowafanya washindwe kuendelea na masomo ." Leo Novemba 15, 2019 Bunge hilo linatarajiwa kuahirishwa baada ya kujadili mpango wa maendeleo ya Taifa kwa mwaka ujao wa fedha. Serikali kujenga mabweni ili wanafunzi wasipate mimba.