Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 15 .07.2019: Harry Maguire, Lewis Dunk, Kieran Tierney, Leroy Sane Manchester United inalipa £80m kumsajili Harry Maguire Manchester United imeafikiana na Leicester makubaliano ya thamani ya £80m kumsajili Harry Maguire na kumfanya kuwa mlinzi mwenye thamani kubwa katika historia. United italipa £60m kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 26 - atakayefanyiwa ukaguzi wa kiafya leo Jumatatu - na £20m za ziada katika siku zijazo. (Sun) Leicester inatarajiwa kuijaza nafasi ya Maguire kwa kumsajili mchezaji wa Brighton Lewis Dunk, baada ya kuafikiana kwa mkataba wa thamani ya £45m kwa mchezaji huyo wa miaka 27. (Sun) Celtic imekataa ombi la Arsenal la hivi karibuni linalokisiwa kuwa na thamani ya £25m - ili kumsajili beki wa kushoto mwenye miaka 22 Kieran Tierney. (Sky Sports) Manchester City inaamini Leroy Sane ataisusia Bayern Munich iwapo itawasilisha ombi la kumsajili winger huyo wa Ujerumani mwenye miaka 23. (Daily M...