Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya USHOGA

​Papa Francis azungumza juu ya "itikadi ya jinsia"

Papa Francis alikariri upinzani wake dhidi ya watu waliobadili jinsia siku ya Ijumaa, akionya kwamba ni “itikadi hatari” na akisema kwamba wafuasi wake hawana akili ikiwa wanaamini wako kwenye “njia ya maendeleo.”  "Fikra za kijinsia, leo, ni mojawapo ya ukoloni hatari zaidi wa kiitikadi," papa alisema katika mahojiano na gazeti la La Nacion la Ajentina. “Kwa nini ni hatari? Kwa sababu inafifisha tofauti na thamani ya wanaume na wanawake.”  Papa amerudia mara kwa mara kupinga nadharia ya jinsia kwa miaka mingi, hata kama amesisitiza haja ya kuwakaribisha na kutoa huduma ya kichungaji kwa watu waliobadili jinsia.

Waafrika Kusini waandamana kisa Makonda

Wananchi nchini Afrika Kusini wameandamana mpaka ubalozi wa Tanzania, wakipinga kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kukataza vitendo vya ushoga na usagaji kwenye mkoa wake. Wananchi hao ambao idadi yao haikujulikana kwa mara moja, pia wamemtaka Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuingilia kati suala hilo, ikiwezakana awape kibali wananchi hao (mashoga) ambao wametajwa kuwa maisha yao yapo hatarini, waweze kuishi Afrika Kusini. “ Rais Ramaphopsa, tunakuita ili utambue hali iliyopo sasa Tanzania, kunyanyaswa kwa haki za binadamu na uhuru wa binadamu, mwambie Makonda kuwa haukubali hiki kitu, tunakutaka uwape hifadhi watu hawa  wa Tanzania, ambao wapo katika hatari ya kuporwa uhuru wao, tunakutaka uchukue hatua kama katiba yetu inavyosema na kitendo chako cha kutetea haki za binadamu ”, walisikika waandamani hao kwenye ujumbe wao. Ikumbukwe kwamba hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alianzisha kampeni ya kukamata watu wanaojihusisha na...

Tanzania yawatimua mawakili 3 wa Afrika Kusini kwa ''kukuza mapenzi ya jinsia moja

MTEULE THE BEST'' Tanzania imewafurusha mawakili watatu wa Afrika Kusini waliokamatwa wiki hii wakituhumiwa kwa kukuza mapenzi ya jinsia moja. Walikuwa miongoni mwa watu 13 waliokamatwa katika hoteli moja mjini Dar es Salaam . Waandalizi wa mkutano huo wanasema kwamba mkutano huo ulikuwa umeitishwa kujadili iwapo wakabiliane na uamuzi wa serikali ya Tanzania kuzuia utoaji wa baadhi ya huduma za afya. Majina ya wapenzi wa jinsia moja kutotangazwa hadharani Tanzania Wapenzi 3 wa jinsia moja watakiwa kuripoti polisi Tanzania Zaidi ya wanaume 40 wapenzi wa jinsia moja kufikishwa mahakamani Nigeria Tanzania yasimamisha huduma za vituo 40 vya afya Mapema mwaka huu, serikali ilipiga marufuku baadhi ya kliniki za kibinafsi kutotoa huduma za ugonjwa wa HIV na ukimwi ikisema zilikuwa zikukuza mapenzi ya jinsia moja ambayo ni haramu nchini Tanzania. Hatahivyo, Sibongile Ndashe anasema kuwa walikuwa hawana haki ya kuwakamata na ameishtumu mamlaka ya Dar es Salaam kwa kuwakamata ...