Somo la Kupaa kwa Yesu na Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu Utangulizi Baada ya Yesu kufufuliwa kutoka kwa wafu, yeye alijidhihirisha kwao, baada ya mateso yake, kwa dalili nyingi, akiwatokea siku arobaini, akinena habari za ufalme wa Mungu. Matendo 1:3 Wanafunzi walipata uthibitisho usio na shaka kwamba Yesu alikuwa amefufuka kweli. Hili lilikuwa lazima, kwa sababu kila mmoja wao angeteseka sana kwa ajili ya Yesu. Haiwezekani kuvumilia mateso mengi kwa kitu ambacho huna uhakika nacho au ambacho unajua ni uwongo! Kupaa Baada ya zile siku arobaini, Yesu alikutana na wanafunzi wake na kuwaambia: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.” Mathayo 28:18 Yesu alikuwa amemshinda Shetani na kumponda kichwa (akitimiza ahadi ambayo Mungu alimpa Hawa kwamba uzao wake ungeponda kichwa cha nyoka) Aliendelea: "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa...