Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kupaa kwa Yesu na Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu



Somo la Kupaa kwa Yesu na Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu

Utangulizi

Baada ya Yesu kufufuliwa kutoka kwa wafu, yeye

     alijidhihirisha kwao, baada ya mateso yake, kwa dalili nyingi, akiwatokea siku arobaini, akinena habari za ufalme wa Mungu.
     Matendo 1:3

Wanafunzi walipata uthibitisho usio na shaka kwamba Yesu alikuwa amefufuka kweli. Hili lilikuwa lazima, kwa sababu kila mmoja wao angeteseka sana kwa ajili ya Yesu. Haiwezekani kuvumilia mateso mengi kwa kitu ambacho huna uhakika nacho au ambacho unajua ni uwongo!
Kupaa

Baada ya zile siku arobaini, Yesu alikutana na wanafunzi wake na kuwaambia:

     “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.”
     Mathayo 28:18

Yesu alikuwa amemshinda Shetani na kumponda kichwa (akitimiza ahadi ambayo Mungu alimpa Hawa kwamba uzao wake ungeponda kichwa cha nyoka) Aliendelea:

     "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi."
     Mathayo 28:19-20

Aliwaambia wapeleke habari njema ya wokovu katika Yesu kwa watu wote duniani kote. Ahadi ya Mungu kwa Abrahamu, kwamba dunia yote ingebarikiwa kupitia uzao wake, ilikuwa inaenda kutimizwa. Kila mtu aliyemwamini Yesu anapaswa kubatizwa. Ubatizo ni kuoga kwa utakaso kwa jina la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu. Wale wanaobatizwa wanakuwa sehemu ya mwili wa Yesu Kristo, kanisa.

Yesu aliendelea kusema:

     "Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."
     Mathayo 28:20

Aliahidi kwamba nguvu za Roho Mtakatifu zingewajia. Hangewaacha wanafunzi wake peke yao bali kutuma Roho wake kuwaongoza na kuwafundisha.

     Naye alipokwisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, aliinuliwa, na wingu likamchukua kutoka machoni pao. Na walipokuwa wakikaza macho mbinguni alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao waliovaa mavazi meupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Yesu huyu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni; atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni."
     Matendo 1:9-11

Kumngoja Roho

Wanafunzi waliambiwa waende Yerusalemu wangojee huko Roho Mtakatifu aje. Lilikuwa ni kundi kubwa kuliko wale wanafunzi kumi na wawili tu:

     Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja kusali, pamoja na wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.
     Matendo 1:14

Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu

Siku kumi baadaye ilikuwa sikukuu ya Pentekoste, na Wayahudi kutoka sehemu nyingi walikuwa wamekuja kusherehekea sikukuu hiyo ya mavuno. Wanafunzi na wafuasi wengine wa Yesu, jumla ya watu 120, walikuwa wamekusanyika pamoja katika chumba kimoja huko Yerusalemu.

     Ghafla, sauti kama ya upepo mkali ikivuma kutoka mbinguni, ikajaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Na zikawatokea ndimi zilizogawanyika kama za moto, zikakaa juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine kama Roho alivyowajalia kutamka.
     Matendo 2:2-4

     Na sauti hii umati wa watu ukakusanyika, wakashangaa, kwa sababu kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.
     Matendo 2:6

Hawa walikuwa ni Wayahudi kutoka sehemu mbalimbali za dunia na walichanganyikiwa kabisa kwamba watu hawa wasio na elimu wangeweza kusema nao kwa lugha zao wenyewe.

     Watu wote wakashangaa na kufadhaika wakiambiana, "Hii ina maana gani?" Lakini wengine wakadhihaki wakisema, "Wamelewa divai mpya."
     Matendo 2:12-13

Roho Mtakatifu alikuwa amekuja! Aliwawezesha waamini ‘kutangaza maajabu ya Mungu’ katika lugha za watu waliokuwapo. Lakini watu wengine hawakuelewa, na Petro aliona fursa nzuri ya kuhubiri Injili. Alieleza jinsi Yesu alivyokuja duniani ili kufa kwa ajili ya dhambi za wote wanaomtumaini. Watu wengi walimwuliza afanye nini ili waokolewe. Alisema:

     "Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu."
     Matendo 2:38

Siku hiyo, watu elfu tatu walitubu na kubatizwa. Waumini walishika

     wakihudhuria Hekaluni pamoja na kuumega mkate nyumbani mwao, wakapata chakula chao kwa furaha na ukarimu wa mioyo yao, wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Na Bwana akawaongeza siku kwa siku wale waliokuwa wakiokolewa.
     Matendo 2:46-47

Kazi ya Roho Mtakatifu katika Maisha ya Mwamini

Roho ilipomiminwa juu ya wanafunzi wa Yesu, walibadilika na kuwa watu wenye ujasiri, waliojaa imani na furaha. Hii ni kazi ya Roho Mtakatifu - anabadilisha mioyo ya wale wanaoweka tumaini lao kwa Yesu. Mmoja wa mitume wa Yesu alielezea kama matunda yanayokua katika maisha ya waumini:

     Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, wema, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
     Wagalatia 5:22

Wakati huo huo, mambo kama vile wivu, hasira, kijicho na tamaa ya ubinafsi vitafifia. Mwamini anabadilishwa kutokana na uwepo wa Roho Mtakatifu katika maisha yake!

Jambo la pili analofanya Roho Mtakatifu ni kukusaidia kuelewa ukweli kuhusu Yesu: Yesu ni nani na amefanya nini.

     Naye atakapokuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, bali yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
     Yohana 16:13

Kila mwamini pia hupokea karama moja au zaidi kutoka kwa Roho Mtakatifu inayomwezesha kuwatumikia watu wengine na kumtumikia Mungu. Miongoni mwa karama za Roho Mtakatifu ni: kutabiri, kufundisha, kutumikia, kutia moyo, kutoa au kuongoza (Warumi 12:6-8; 1 Wakorintho 12:4-11). Karama hizi zote hutumika kusaidia kujengana na kukua karibu na Mungu.

Wafuasi wa Kristo hawashindani na damu na nyama, bali ni juu ya majeshi ya pepo wabaya (Waefeso 6:10-18). Kwa sababu Roho Mtakatifu anafanya kazi katika maisha ya waumini hatuhitaji kuogopa nguvu hizo. Mungu huwapa wafuasi wa Yesu silaha za kiroho ili kusimama dhidi ya hila za shetani. Yesu alikuwa na ushindi juu ya shetani na tunashiriki ushindi huu ikiwa tunamwamini.


Pointi Kuu
     Yesu alienda mbinguni, lakini siku moja atarudi.

     Yesu yuko pamoja nasi hadi mwisho wa nyakati kwa njia ya Roho wake.

     Roho Mtakatifu hubadilisha moyo wa mwamini.

     Roho Mtakatifu huwawezesha waumini kumtumikia Mungu.

mteulethebest

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...