Mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums Maxence Melo Jukwaa maarufu nchini Tanzania JamiiForums hatimaye limefunguliwa baada ya kufungwa kwa takriban wiki mbili, kufuatia kuanza kutekelezwa kwa sheria mpya za mtandaoni nchini humo. Kulingana na ujumbe uliosambazwa katika ukurasa wa Twitter wa tovuti hiyo, kwa sasa ujumbe ambao ulikuwa umepakiwa awali unaweza kusomwa. Mkurugenzi wa mtandao huo Maxence Melo aliyekuwa akijibu ujumbe wa mmoja wa wateja wake katika mtandao wa Twitter amenukuliwa katika ujumbe huo akisema hata hivyo kwamba watumiaji wa mtandao huo hawawezi kuchapisha ujumbe mpya kwa sasa. Aliongezea kusema kwamba hatua za kurejesha operesheni zote kama ilivyokuwepo mwanzo zinaendelea. Kwa sasa habari za mtandao huo ambazo zilikuwa zimechapishwa kuanzia 10 Juni kwenda nyuma kabla ya kufungwa kwa jukwaa hilo zinaweza kusomwa. Hata hivyo haijajulikana ni lini operesheni kamili za mtandao huo zitaanza ili wasomaji kuanza kuchangia. Walipofunga mtandao huo...