Declan Rice Manchester United kutangaza dau la usajili la pauni milioni 50 ili kumnasa kiungo kinda wa West Ham Declan Rice,20. (Irish Independent) Rice, amesema kujiunga na West Ham ulikuwa uamuzi bora kabisa aliowahi kuufanya baada ya Chelsea kumtema akiwa na miaka 14. (Standard) Beki wa kushoto wa Ajax Nicolas Tagliafico, 26, amesema kuwa mwisho wa msimu huu utakuwa ni muda muafaka wa kuhamia kwenye Ligi ya Premia. Beki huyo raia wa Argentina anawindwa na Arsenal. (Mirror) Kocha msaidizi wa Manchester United Mike Phelan amesema kiungo wa klabu hiyo Paul Pogba, 26, "bado hajamaliza kazi yake" na anamtaka mchezaji huyo kusalia Old Trafford. (Telegraph) Paul Pogba anaendeleakugonga vichwa vya habari akihusianishwa na uhamisho kwenda Real Madrid mwishoni mwa msimu. Jarida la 'France Football' la nchini Ufaransa klinamshawishi Pogba kuhama Old Trafford na kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu. (France Football - in French) Rais wa Barcelona Josep Maria ...