Beki wa zamani wa Real Madrid Michel Salgado anaamini mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 24, ndiye anayelengwa na klabu hiyo msimu huu baada ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 26. (Talksport)
Chelsea inajaribu kuipiku Manchester City katika kumsaini kiungo wa kati wa Lazio na Itali Jorginho, 26. (Manchester Evening News)
City pia imembishia hodi kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Mateo Kovacic, 24, huku wakiwa na wasiwasi kuhusu kumtia mkobani Jorginho. (Mirror)
Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 29, anatarajiwa kusalia na klabu hiyo licha ya kuhusishwa na uhamisho (Bild)
Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Roma Monchi anasema kuwa ataangazia maombi ya kumuuza kipa wa Brazil Alisson lakini kufikia sasa hakuna klabu iliowasilisha ombi la kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (FourFourTwo)
Manchester United na Real Madrid wamekutana na maafisa kutoka Lazio kujadili uhamisho wa kiungo wa kati wa Serbia mwenye umri wa miaka 23 Sergej Milinkovic-Savic. (Il Messaggero - via Talksport)
Southampton ina matumaini ya kukamilisha mkataba wa £18m kumnunua beki wa Borussia Monchengladbach na Denmark Jannik Vestergaard, 25. (Daily Echo)
Newcastle United ina matumaini ya kumsajili kwa mkopo winga wa Chelsea Kenedy kabla ya klabu hiyo kuelekea Ireland baadaye wiki hii. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Brazil anaelekea Tyneside kukamilisho uhamisho wa mkopo (Newcastle Chronicle)
Borussia Dortmund inapanga kutumia fedha walizopata baada ya kumuuza mshambuliaji wa Ukraine Andriy Yarmolenko aliyeelekea West Ham ili kusaidia kufadhili uhamisho wa Wilfried Zaha, 25, kutoka Crystal Palace ambaye amevutia hamu kutoka klabu za Tottenham na Everton baada ya kukataa mkataba mpya katika klabu ya Selhurst Park. (Sun)
Mkufunzi mpya wa Everton Marco Silva yuko tayari kumnunua Zaha, 25. (Mirror)
Juventus imeiambia Liverpool inaweza kumsaini winga wa Croatia Marko Pjaca, 23, msimu huu kwa dau la £22m. (Gazzetta dello Sport - via Talksport)
Ombi la Liverpool la kutaka kumnunua mchezaji wa Croatia na Besikitas Domagoj Vida ,29, kwa dau la 18m limekataliwa (90min)
West Ham huenda ikamsajili mshambuliaji wa Sevilla Franco Vazquez, 22, huku klabu hiyo ya Uhispania ikisubiri kumuuza mchezaji huyo wa Itali kwa dau linalovutia. (Sport Witness)
Hull imekubaliana na West Ham kuhusu beki wa Uingereza Reece Burke, 21. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Manchester City Mario Balotelli atakuwa mchezaji anayepokea donge nono zaidi katika klabu ya Marseille atakapokamilisha uhamisho wake kutoka Nice katika siku chache zijazo. (RMC - via Talksport)
West Ham United imewasilisha ombi lililovunja rekodi ya usajili katika klabu hiyo kwa mshambuliaji wa Lazio na Brazil Felipe Anderson, 25. (Goal.com - via Calciomercato)
Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery yeye mwenyewe alimshawishi kiungo wa kati wa Lorient na Ufaransa Matteo Guendouzi, 19, kujiunga na Arsenal badala ya Paris St-Germain Borussia Dortmund. (L'Equipe - via Metro)
Kiungo wa kati wa Liverpool Allan Rodrigues de Souza, 21, ameelekea Marekani na klabu ya Ujerumani ya Eintracht Frankfurt kabla ya uhamisho wake wa mkopo katika klabu hiyo ya Bundesliga club. (Liverpool Echo)
Chelsea, Tottenham, Manchester City, Barcelona na Inter Milan huenda wakamkosa mshambuliaji wa Nigeria ,20, Taiwo Awoniyi, ambaye anatarajiwa kutia saini mkataba mpya na Liverpool ambao utamfanya kuelekea Monaco kwa mkopo (Teamtalk)
Newcastle United imejiunga katika kinyang'anyiro cha kumsaini kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, 23. (A Bola - via Sportslens)
Manchester United wametuma maskauti kumtazama mshambuliaji wa klabu ya Molde na Norway, 17, Erling Haaland, mwanawe kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City na Leeds Alf-Inge Haaland. (Mirror)
Newcastle na Tottenham huenda wakamkosa mshamnbuliaji wa Nice na Ufaransa Alassane Plea huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akitarajiwa kuelekea katika klabu ya ligi ya Bundesliga Borussia Monchengladbach. (RP-Online)
Galatasaray imeanza mazungumzo ya kutaka kumsajili winga wa Nigeria na Everton Henry Onyekuru, 21, kwa mkopo. (Liverpool Echo)
Mkufunzi wa Aston Villa Steve Bruce anasema kuwa hali ya kifedha ya klabu hiyo inamaanisha kwamba wachezaji kama vile kiungo wa kati wa Uingereza Jack Grealish, 22, wataondoka msimu huu. (Sky Sports
Maoni