Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya PUTIN

Urusi iliepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe - Putin

Rais wa Urusi Vladimir Putin akitoa hotuba kwa vitengo vya Wizara ya Ulinzi, Walinzi wa Urusi, Wizara ya Mambo ya Ndani, FSB na FSO. Rais wa Urusi aliwasifu wanajeshi na maafisa wa usalama kwa uamuzi wao wakati wa maasi ya Wagner Group wiki iliyopita Jeshi la Urusi na vyombo vyake vya kutekeleza sheria vilizuia mzozo mkubwa wa kijeshi wa ndani nchini humo wiki iliyopita, Rais Vladimir Putin amesema, akimaanisha uasi uliotimizwa na mkuu wa Wagner Group Evgeny Prigozhin. "Kwa kweli, umesimamisha vita vya wenyewe kwa wenyewe, ukitenda kwa usahihi na kwa ushirikiano," aliambia kikundi cha wanachama wa huduma, ambao walikusanyika Kremlin Jumanne kupokea mapambo ya serikali kwa jitihada zao Ijumaa na Jumamosi iliyopita. Mwitikio wa watu, ambao usalama wa Urusi unategemea, uliwezesha ulinzi wote muhimu na mifumo ya serikali kuendelea kufanya kazi, rais alisema. Alibainisha kuwa hakuna vitengo vilivyoondolewa kutoka mstari wa mbele wa operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine. ...

Kim wa Korea Kaskazini Anataka Nyenzo Zaidi ya Nyuklia - Ripoti

  Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amedai nyenzo zaidi za kiwango cha nyuklia ili uwezekano wa kutengeneza silaha za kimbinu zaidi, kulingana na ripoti ya Jumanne kutoka kwa chombo cha habari cha serikali KCNA.  Ripoti hiyo iliongeza kuwa wanasayansi wakuu walimweleza Kim juu ya teknolojia ya hivi punde ya makombora ya nyuklia huku pia akichunguza mipango iliyoanzishwa ya kukabiliana na nyuklia.  Wachambuzi wanasema hati ya ulinzi ya Korea Kusini ya kila baada ya miaka miwili iliyotolewa mwezi uliopita ilidai kuwa Kaskazini tayari imekusanya takriban kilo 70 za plutonium ya kiwango cha silaha - zinazotosha kuzalisha kati ya silaha za nyuklia 9-18.

Putin Azungumuzia shambulio la kigaidi New Zealand

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa sababu kuu ya shambulizi la misikiti miwili New  Zealand ni kuitikisa nchi hiyo Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa sababu kuu ya shambulizi la misikiti miwili New  Zealand ni kuitikisa nchi hiyo. Katika mkutano wake na wawakilishi wa jamii katika Crimea na Sevastopol, Putin amejadili mashambulizi ya kigaidi juu ya misikiti huko New Zealand. Putin alionyesha heshima yake kwa wale waliouawa katika shambulio hilo. "Lengo la mashambulizi makubwa ya kigaidi huko New Zealand ni kuitingisha nchi." alisema. Akionyesha kuwa vitendo vya kigaidi ni hatari kwa kila nchi, Putin amesema kuwa Urusi haitaruhusu mashambulizi hayo. Katika mji wa Christchurch, New Zealand, wakati wa sala ya Ijumaa, watu 50 waliuawa na gaidi aliyoshambulia misikiti miwili.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro Marekani inapanga njama ya kumuua na kupindua serikali yake

John Bolton amepewa jukumu la kupanga jinsi ya kuniangamiza' Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akizungumza na wanahabari mjini Caracas Desmba 12,2018 Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amedai kuwa Marekani inapanga njama ya kumuua na kupindua serikali yake. Amewaambia wanahabari kuwa mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani John Bolton, anahusuka moja kwa moja na njama hiyo japo hakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai hayo. Rais Trump amemtaja Maduro kama kiongozi wa kiimla na kumwekea vikwazo. Mapema wiki hii maafisa wakuu wa Urusi na Marekani walijibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika Kusini. Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumatatu katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa kisoshialisti wa Venezuela Nicolás Maduro ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo. Ndege hizo mbili zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia. Madur...

Kitambulisho cha Vladimir Putin akiwa jasusi wa KGB chapatikana Ujerumani

Vladimir Putin alikuwa na umri wa miaka 33 alipopewa kitambulisho hicho Kitambulisho cha Vladimir Putin alichopewa kama jasusi Ujerumani alipokuwa anafanya kazi kama jasusi wa Urusi kimepatikana katika makavazi mjini Dresden. Rais huyo wa Urusi amekuwa mara kwa mara akisema anajivunia kazi aliyoifanya akiwa kama jasusi wa idara ya ujasusi ya Urusi wakati huo ikifahamika kama KGB jijini Dresden miaka ya 1980. KGB kwa kirefu ni Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti (Kamati/Idara ya Usalama wa Taifa) Putin, wakati huo, alipewa kitambulisho na idara ya ujasusi ya Ujerumani Mashariki ambayo wakati huo ilikuwa chini ya Muungano wa Usovieti (USSR). Idara ya ujasusi ya Ujerumani Mashariki ilifahamika kama Stasi, lakini kwa kirefu ni Ministerium für Staatsicherheit kwa maana ya maajenti wa Wizara ya Usalama wa Taifa. Kitambulisho cha Stasi alichokitumia Putin kimegunduliwa wakati wa uchunguzi kuhusu ushirikiano wa karibu uliokuwepo kati ya KGB na Stasi. Putin ambaye wakati huo...

Rais Donald Trump kukutana na Rais Putin katika mkutano wa G-20

Rais wa Marekani Donald Trump afahamisha kuwa atakutana na rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano wa G-20, mkutano ambao unatarajiwa kufanyika nchini Argentina.  Mkutano wa G-20 utafanyika mwishoni mwa Novemba.  Rais Trump ametoa taarifa hiyo katika mahojiano aliofanya na waandishi wa habari mjiniikulu mjini Washington.  Trump atashiriki pia katika hafla ya maadhimisho ya kusitishwa vita  ya mwaka 1918 mjini Paris nchini Ufaransa Novemba 10 n a 11

Arkady Babchenko – mtu aliyerejea kutoka kwa wafu

Mkosoaji wa serikali ya Urusi Arkady Babchenko ni mtu aliyerejea kutoka kwa wafu. Hivyo ndivyo ilivyoonekana mjini Kiev wakati maafisa waliandamana naye kuzungumza kuhusu "uchunguzi wa mauaji". Mara akajitokeza tena. Mtu ambaye tayari alikuwa ametolewa salamu za rambirambi kutoka kila sehemu na ambaye jina lake liliongezwa kwenye orodha ya kumbukumbu ya wanahabari mjini Moscow saa chache kabla. Arkady Babchenko alirejea kutoka kwa wafu akiandamana na mkuu wa ujasusi wa Ukraine na mwendesha mashitaka mkuu. Mwanahabari huyo alikuwa ametangazwa kuuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake mjini Kiev. Babchenko mwenye umri wa miaka 41 alivishukuru vikosi vya usalama vya Ukraine kwa kuyaokoa maisha yake kabla ya kumuomba radhi mkewe kwa kumuweka katika hali ngumu kama hiyo. "Nnavyojua ni kuwa operesheni hii ilipangwa kwa zaidi ya miezi miwili, lakini nilifahamishwa mwezi mmoja uliopita. Katika mwezi huu niliona jinsi maafisa walivyofanya kazi, kama walivyofukua mambo ka...

Uholanzi, Australia zaituhumu Urusi kuidungua ndege ya MH17

Uholanzi imeiambia Urusi kwamba itaishitaki kwa jukumu lake katika kuangushwa kwa ndege ya Malaysia yenye nambari za safari MH17 tarehe 17 Julai 2014 baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa kombora la Urusi ndio lililotumika. MH17 ilidunguliwa ikiwa katika eneo linalodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi mashariki mwa Ukraine wakati ikiwa angani kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur, na kuuwa watu wote 298 waliokuwemo, ambapo karibu theluthi mbili walikuwa raia wa Uholanzi. Timu ya wachunguzi wa kimataifa ilisema siku ya Alhamisi kuwa mfumo wa makombora wa "Buk" uliotumiwa kuidungua ndege hiyo ya abiria ulitoka kwenye brigade ya 53 ya mashambulizi ya ndege, yenye makao yake katika mji wa Magharibi mwa Urusi wa Kursk. "Hii ndiyo mara ya kwanza taifa makhsusi kunyooshewa kidole," waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri. "Tunaitwika lawama Urusi kwa ushiriki wao katika kupe...

Je Ukraine itaenedelea kupokea gesi kutoka Urusi?

Rais wa Urusi Vladimir Putin amemwambia kansela Angela Merkel kwamba gesi ya asili ya Urusi inaweza kupelekwa kwenye nchi jirani ya Ukraine iwapo yatakuwepo manufaa ya kiuchumi kwa Urusi. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Urusi Vladimir Putin kwenye mazungumzo yao wamejadiliana kuhusu mgogoro wa nchini Ukraine, wakati ambapo Urusi inaongeza ukubwa wa bomba lake la gesi ya asili kwenda moja kwa moja hadi nchini Ujerumani, bila kupitia Ukraine. Rais Putin na Waziri wake Mkuu Dmitry Medvedev walimkaribisha Kansela Merkel katika makao ya rais ya majira ya kiangazi yaliyopo katika jiji la kusini mwa Urusi la Sochi, kansela Merkel ndiye aliyeongoza vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi wakati nchi hiyo ilipolitwaa jimbo la Crimea miaka minne iliyopita. Lakini katika miezi ya hivi karibuni, Ujerumani ilitoa idhini yake kwa Urusi kuweza kutanua bomba lake la gesi la Nord Stream, ambalo litasafirisha gesi ya asili hadi nchini Ujerumani licha ya Ukraine kuupinga mra...