Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kitambulisho cha Vladimir Putin akiwa jasusi wa KGB chapatikana Ujerumani




Vladimir Putin alikuwa na umri wa miaka 33 alipopewa kitambulisho hicho

Kitambulisho cha Vladimir Putin alichopewa kama jasusi Ujerumani alipokuwa anafanya kazi kama jasusi wa Urusi kimepatikana katika makavazi mjini Dresden.

Rais huyo wa Urusi amekuwa mara kwa mara akisema anajivunia kazi aliyoifanya akiwa kama jasusi wa idara ya ujasusi ya Urusi wakati huo ikifahamika kama KGB jijini Dresden miaka ya 1980.

KGB kwa kirefu ni Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti (Kamati/Idara ya Usalama wa Taifa)

Putin, wakati huo, alipewa kitambulisho na idara ya ujasusi ya Ujerumani Mashariki ambayo wakati huo ilikuwa chini ya Muungano wa Usovieti (USSR).



Idara ya ujasusi ya Ujerumani Mashariki ilifahamika kama Stasi, lakini kwa kirefu ni Ministerium fĆ¼r Staatsicherheit kwa maana ya maajenti wa Wizara ya Usalama wa Taifa.

Kitambulisho cha Stasi alichokitumia Putin kimegunduliwa wakati wa uchunguzi kuhusu ushirikiano wa karibu uliokuwepo kati ya KGB na Stasi.

Putin ambaye wakati huo aikuwa na cheo cha meja katika KGB alipewa kitambulisho hicho kwama 1985 na kilimuwezesha kuingia kwenye afisi za Stasi, lakini si lazima iwe kwamba alifanya ujasusi kwa niaba yao.

Kupitia taarifa iliyotolewa Jumanne, maafisa wa Wakala wa Nyaraka za Stasi (BStU) walisema Bw Putin "alipokeza kitambulisho hicho ili kumuwezesha kufanya kazi zake za KGB kwa ushirikiano na Stasi."

Majasusi wa Stasi walifahamika sana kwa njia zao kali za ujasusi na jinsi walivyowapeleleza raia wa kawaida.

Wakati mwingine waliwalazimisha watu wa kawaida kutoa habari kuhusu raia wenzao, hata wa karibu.

"Utafiti wa sasa haujatoa ishara zozote kwamba Vladimir Putin alifanyia kazi Stasi," taarifa ya BStU imesema.


Mihuri hii ni ishara ya miaka ya Bw Putin alivyoshirikiana na Stasi mjini Dresden kwa miaka kadha


Bw Putin alitia saini kama "Wladimir Putin", jinsi linavyoandikwa jina lake kwa Kijerumani

Bw Putin, alizaliwa Leningrad (mji ambao kwa sasa huitwa St Petersburg) na kwa sasa ana miaka 66.

Alitumwa Ujerumani Mashariki kama jasusi mwaka 1985 akiwa na miaka 33.

Mabinti zake wawili walizaliwa akiwa Ujerumani.



Putin alihudumu kama jasusi wa KGB mjini Dresden hadi Desemba 1989 pale utawala wa Kikomunisti wa Ujerumani Mashariki ulipoporomoka kutokana na maandamano ya kutetea demokrasia.

Kitambulisho chake cha Stasi kiliidhinishwa upya kila miezi mitatu, kama inavyoonyeshwa kwenye mihuri kwenye kitambulisho hicho.

Haijafahamika ni kwa nini alikiacha kitambulisho hicho kwenye nyaraka za Stasi mjini Dresden


Jengo hili lilikuwa makao makuu ya KGB mjini Dresden wakati wa Vita Baridi

Alikuwepo waandamanaji walipozingira na kutwaa udhibiti wa makao makuu ya Stasi mjini Dresden. Maafisa wa usalama wa kikomunisti waliokuwa wanalinda makao makuu hayo walikuwa karibu sana kuwafyatulia waandamanaji hao risasi siku hiyo 5 Desemba 1989.


Wakazi wa Berlin Mashariki iliyokuwa chini ya Ujerumani Mashariki walikuwa tayari wameuvunja na kuanza kuubomoa ukuta wa Berlin Novemba.

Bw Putin alikuwa anazungumza Kijerumani kwa ufasaha wakati huo na baadaye alisema aliitwa binafsi kujaribu kuwatuliza watu waliokusanyika na kuzingira afisi za KGB mjini humo.

Aliwaonya kwamba ilikuwa ni ardhi ya Muungano wa Usovieti.


Vladimir Putin akiwa na sare ya KGB

Wakati akifanya kazi na KGB mjini Dresden, Putin alipandishwa cheo hadi kuwa luteni kanali.

Mwaka 1989, alitunukiwa nishani ya shaba na Ujerumani Mashariki ikiwa bado chini ya utawala wa kikomunisti kwa "huduma yake na uaminifu wake katika kulitumikia Jeshi la Taifa la Wananchi", inasema tovuti ya ikulu ya Urusi, Kremlin.

Ujerumani Mashariki kirasmi ilifahamika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani (GDR).

Baada ya kurejea Urusi, Bw Putin alipanda cheo na kuwa mkuu wa Idara ya Usalama wa Dola (FSB, kwa Kiingereza Federal Security Service) ambayo ndiyo iliyochukua nafasi ya KGB.

Alifanyia kazi meya wa St Petersburg kati ya 1990 na 1996, na baadaye akapanda cheo kisiasa hadi alipoteuliwa rais wa Urusi mwaka 2000.

Juni 2017, Putin alifichua kwamba kazi yake akiwa KGB ilijumuisha "kukusanya habari za kijasusi kwa njia haramu."


Akizungumza na runinga ya taifa ya Urusi, alisema majasusi wa KGB walikuwa watu wenye "sifa za kipekee, kujitolea kwa hali ya juu na watu tabia za kipekee."

Mkataba wa siri kati ya KGB na Stasi ambao BBC ilibahatika kuuona unaonyesha wakati mmoja KGB ilikuwa na maajenti 30 waliofanya kazi na Stasi Ujerumani Mashariki.


Putin akiwa katika mgahawa mmoja Dresden mwaka 2006

Vladimir Putin akiwa Dresden mwaka 2006

Msemaji wa ikulu ya Urusi Dmitry Peskov amepuuzilia mbali uzito wa taarifa za kupatikana kwa kitambulisho hicho cha Putin alichopewa na Stasi.



"KGB na Stasi walikuwa mashirika mawili ya ujasusi yaliyokuwa na ushirikiano hivyo hauwezi kufutilia mbali uwezekano kwamba walibadilishana vitambulisho kama hivyo," 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...