Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva na moja ya kiongozi katika kundi la Tip Top Connection, Madee Alli 'Seneda' ameelezea tamaa yake juu ya kumiliki ndege yake binafsi katika maisha yake.
Msanii, Madee (kushoto) na Mwanasoka, Mbwana Samatta (kulia)
Madee amesema kuwa ana ndoto ya kumiliki ndege katika maisha yake kiasi cha kumnyima usingizi wake kila siku.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Madee ameandika, "ndoto inayosumbua usingizi wangu," huku akiwa katika picha inayomuonesha akitembea kuelekea kwenye ndege ndogo.
Kauli hiyo ya Madee kuhusu kumiliki ndege inakuja miezi michache baada ya nyota wa soka nchini anayechezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta kueleza matamanio yake juu ya kumiliki ndege yake binafsi.
Septemba 12, Samatta katika ukurasa wake wa Instagram aliandika, "ndoto za kumiliki 'Private Jet' zimeanza baada ya kupiga picha hii, sio kila ndoto inaweza kutimia ila acha vita ianze".
Kwakuwa wote ni watu maarufu katika tasnia tofauti, tusubiri na tuone ni nani kati ya Samatta na Madee atakayekuwa wa kwanza kutimiza ndoto hiyo ya kumiliki ndege binafsi kama walivyoeleza.
Maoni