Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tupolev -160: Ndege za kuangusha mabomu za Urusi zatua Venezuela na kuighadhabisha Marekani




Ndege aina ya Tupolev Tu-160 iliyotua uwanja wa Simón Bolívar Jumatatu

Maafisa wakuu wa Urusi na Marekani wamejibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika Kusini.


Ndege hizo mbili zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.

Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumattau katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa Kisoshialisti wa Venezuela Nicolás Maduro ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo.



Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema kitendo hicho ni sawa na "serikali mbili fisadi kufuja mali ya umma."

Serikali ya Urusi imesema maneno yake hayo "hayafai hata kidogo."


Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa ujumbe wa Youtube wa Минобороны России

Ndege hizo mbili za kivita zenye uwezo wa kusafiri mwendo mrefu bila kutua zilitua katika uwanja wa ndege wa Simón Bolívar viungani mwa mji mkuu wa Venezuela, Caracas, zikiandamana na ndege nyingine mbili za Urusi.

Venezuela na Urusi zimekuwa marafiki kwa muda mrefu na ndege hizo mbili za kivita ziliwahi kutumwa tena taifa hilo mwaka 2008, zikiwa pamoja na manowari moja yenye uwezo wa kurusha makombora.

Ndege hizo zilifika tena Venezuela mwaka 2013.


Waziri wa ulinzi wa VenezuelaVladimir Padrino (wa pili kushoto, mstari wa mbele) aliwalaki Warusi hao

Kitendo cha sasa kimetokea siku chache tu baada ya rais Maduro kukutana na Rais Vladimir Putin mjini Moscow.



Waziri wa Ulinzi wa Venezuela Vladimir Padrino alisema ndege hizo ni sehemu ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Venezuela na mshirika wake Urusi.

"Hili tunalifanya kwa pamoja na marafiki zetu, kwa sababu tuna marafiki duniani ambao hutetea na kuheshimu uhusiano wa usawa."


Njia zinazotumiwa na raia wa Venezuela baada ya kuondoka nchini mwao

"Tunajiandaa kuilinda Venezuela hadi hatua ya mwisho ikilazimu," alisema waziri huyo akionekana kurejelea tuhuma za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali ya nchi hiyo kwamba yapo mataifa yanayotaka kupindua serikali ya nchi hiyo.



Rais Maduro alisema Jumapili kwamba kuna juhudi zinazoendelea kwa sasa "zikiratibiwa moja kwa moja kutoka White House (Marekani) za kuvuruga maisha ya kidemokrasia Venezuela na kutekeleza mapinduzi dhidi ya serikali iliyochaguliwa kikatiba, kidemokrasia na iliyo huru ya taifa letu."

Bw Pompeo alishutumu kitendo cha kutumwa kwa ndege hizo za Urusi kwenye Twitter.

Haki miliki ya pichaTWITTER

Msemaji wa Rais wa Urusi Vladimir Putin, Dmitry Peskov, amesema tamko la Pompeo si la kidiplomasia hata kidogo.

Bw Pompeo hakuwa afisa pekee wa Marekani aliyeshutumu kitendo hicho cha Urusi.


Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Kanali Rob Manning alisema hivi majuzi, Marekani ilituma meli ya jeshi la wanamaji inayotumiwa kama hospitali Amerika Kusini kutoa msaada wa kimatibabu kwa mamilioni ya raia wa Venezuela ambao wameikimbia nchi yao kutokana na mfumko mkubwa wa bei ya bidhaa na huduma na uhaba mkubwa wa bidhaa, chakula na dawa nchini mwao tangu mwaka 2014.


Maelfu ya raia wa Venezuela wamekuwa wakiyakimbia maisha magumu nchini mwao

"Hii ni tofauti sana na Urusi, ambao hatua yao kutatua mgogoro huu wa kibinadamu Venezuela ni kutuma ndege za kuangusha mabomu badala ya msaada wa kibinadamu," amesema Kanali Manning kwa mujibu wa kituo cha habari cha NBC.

Lakini Urusi siyo pekee iliyotuma ndege za kivita katika taifa au mataifa mengine.

Haki miliki ya pichaAFPImage captionMmoja wa marubani wa kijeshi waliosafiri na ndege hizo za Urusi

Marekani pia ilituma ndege za kivita nchini Ukraine, moja ya washirika wake, baada ya uhusiano wake na Urusi kudorora hasa baada ya Urusi kumega eneo la Crimea mwaka 2014.

Urusi ilichukulia hatua ya Marekani na mataifa ya Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi (Nato) ya kujenga ushirikiano wa karibu na Ukraine kwama tisho kwake.

Ndege aina ya Tu (Tupolev)-160 ni za aina gani?

Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES

Hufahamika kama White Swans nchini Urusi (lakini zimepewa jina la utani la Blackjacks na Nato)


Ni ndege zenye mabawa yanayoweza kuyumba-yumba na zinaweza kwenda kwa kasi mara mbili zaidi ya kasi ya sauti


Ndege za kwanza zilizinduliwa mwaka 1981, lakini zikaboreshwa miaka ya 2000


Zinaweza kusafiri umbali wa 12,000km (maili 7,456) bila kutua


Zinaweza kubeba makombora na mabomu ya nyuklia


Zilitumiwa na Urusi katika vita Syria kuanzia mwaka 2015


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...