River Plate Bingwa wa Copa Libertadores, ilikuwa game ya kihistoria Bernabeu
Fainali ya Kombe la Copa Libertadores kati yaRiver Plate na Boca Junior unaweza kuiita fainali ya kusisimua katika soka usiku wa December 9 2018, mvuto wa fainali hiyo unakuja kutokana na kuzikutanisha timu wapinzani ambao wamesabisha kiasi cha game hiyo kushindwa kuchezwa Argentina na kupelekwa katika jiji la Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
Mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mastaa kibao wa soka akiwemo Lionel Messi wa FC Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid, ulimalizika kwa River Plate kupata ushindi wa magoli 3-1, hiyo wanashinda taji hilo kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-3, kwani mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2.
Ubingwa wa Copa Libertadores kwa River Plate unakuwa ni Ubingwa wao wa nne katika historia baada ya kutwaa 1986 kwa mara ya kwanza, 1996 kwa mara ya pili, 2015 kwa mara ya tatu na leo mwaka 2018 wametwaa kwa mara ya nne katika historia na kumuacha Carlos Tevez na wachezaji wenzake wa Boca Junior wakiondoka Santiago Bernabeu vichwa chini
Maoni