MTEULE THE BEST Mkewe rais wa Nigeria Aisha Buhari amesema kuwa mumewe sio mgonjwa sana zaidi ya inavyodhaniwa. Alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema kuwa Muhammadu Buhari mwenye umri wa miaka 74 anaendelea na majukumu yake na kwamba amekuwa akikutana na mawaziri. Kundi moja la watu mashuhuri lilimtaka rais Buhari kuchukua likizo ya matibabu kufuatia wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya. Mnamo mwezi Machi alirudi nchini Nigeria baada ya likizo ya matibabu iliochukuwa wiki saba nchini Uingereza ambapo alitibiwa ugonjwa usiojulikana Wakati aliporudi nyumbani alisema kuwa hajawahi kuwa mgonjwa sana maishani mwake. Rais huyo hajaonekana hadharani kwa kipindi cha wiki moja sasa, na hatua ya kutohudhuria mkutano wa baraza la mawaziri pamoja na ibada ya kila wiki ya Waislamu inayofanyika siku ya Ijumaa, imesababisha uvumi zaidi kuhusu hali yake ya kiafya, kundi hilo la watu 13 limesema katika taarifa. Bi Buhari alishutumiwa na mumewe mwaka uliopita aliposema ka...