Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mkewe rais wa Nigeria Aisha Buhari amesema kuwa mumewe sio mgonjwa sana zaidi ya inavyodhaniwa

MTEULE THE BEST


Mkewe rais wa Nigeria Aisha Buhari amesema kuwa mumewe sio mgonjwa sana zaidi ya inavyodhaniwa.
Alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema kuwa Muhammadu Buhari mwenye umri wa miaka 74 anaendelea na majukumu yake na kwamba amekuwa akikutana na mawaziri.
Kundi moja la watu mashuhuri lilimtaka rais Buhari kuchukua likizo ya matibabu kufuatia wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya.
Mnamo mwezi Machi alirudi nchini Nigeria baada ya likizo ya matibabu iliochukuwa wiki saba nchini Uingereza ambapo alitibiwa ugonjwa usiojulikana
  • Wakati aliporudi nyumbani alisema kuwa hajawahi kuwa mgonjwa sana maishani mwake.
Rais huyo hajaonekana hadharani kwa kipindi cha wiki moja sasa, na hatua ya kutohudhuria mkutano wa baraza la mawaziri pamoja na ibada ya kila wiki ya Waislamu inayofanyika siku ya Ijumaa, imesababisha uvumi zaidi kuhusu hali yake ya kiafya, kundi hilo la watu 13 limesema katika taarifa.
Bi Buhari alishutumiwa na mumewe mwaka uliopita aliposema katika mahojiano ya BBC kwamba hataunga mkono kuchaguliwa tena kwa mumewe hadi pale atakapofanya mabadiliko katika serikali yake akidai kuwa imetekwa na watu wachache.
Na akijibu matamshi hayo ya mkewe bwana Buhari alisema kwamba mkewe anafaa kuwa katika chumba chengine.
Aisha Buhari akimkarisha nyumbani mumewe baada ya kuwasili kutoka kwa likizo ya matibabu nchini UingerezaHakiREUTERS
ImageAisha Buhari akimkarisha nyumbani mumewe baada ya kuwasili kutoka kwa likizo ya matibabu nchini Uingereza
Waziri wa habari Lai Mohammed aliambia BBC kwamba afya ya rais ni swala la kibinafsi na kwamba raia wa Nigeria wamekuwa wakielezwa kuhusu hali yake.
Kundi hilo linashirikisha wanaharakati wenye ushawishi mkubwa akiwemo wakili Femi Falana, mchanganuzi wa maswala ya kisiasa Jibrin Ibrahim na kiongozi wa shirika la Transparence International tawi la Nigeria Anwal Musa Rafsanjani.
Raia hao 13 wanasema kuwa walilazimika kumshauri rais Buhari kusikiza ushauri wa daktari wake wa kibinafsi kwa kuchukua mapumziko ili kuangazia afya yake bila kuchelewa.
Msaidizi wa Bwana Buhari ,Bashir Ahmed alisema kuwa rais alikutana na waziri wa haki Abubakr Malami na maafisa wengine katika jumba la rais siku ya Jumanne ikiwa miongoni mwa majukumu yake.
Wiki iliopita, msemaji wa rais Garba Shehu alisema kuwa bwana Buhari alikuwa akichukua majukumu yake polepole huku akiendelea kupona kufuatia kipindi kirefu cha matibabu nchini Uingereza.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...