Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya NIGERIA

Tanzania yavunja mkataba na kocha Emmanuel Amunike

Amunike alipewa kibarua cha kuinoa Tanzania maarufu kama Taifa Stars mwezi Aprili 2018. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo Jumatatu Julai 8 limetangaza kusitisha mkataba na kocha Emmanuel Amunike. Taarifa fupi iliyotolewa na TFF inadai kuwa Amunike amekubaliana na TFF kusitisha mkataba huo. Shirikisho hilo pia limesema pia litatangaza Kocha wa muda atakaekiongoza Kikosi cha Timu ya Taifa kwa mechi za CHAN. "Makocha wa muda watatangazwa baada ya Kamati ya Dharura ya Kamati ya Utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019," inasema taarifa ya TFF. Mchakato wa kutafuta Kocha mpya umeanza mara moja. Amunike alipewa kibarua cha kuinoa Tanzania maarufu kama Taifa Stars mwezi Aprili 2018. Atabakia kwenye historia ya mpira Tanzania kwa kuingoza nchi hiyo kufuzu kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya miaka 39. Kabla ya hapo alinyanyua Kombe la Dunia 2015 akiwa kocha wa timu ya vijana wa chini ya miaka 17 Nigeria. Kocha hu...

Serengeti Boys” itashiriki kwenye mashindano maalumu ya CAF na UEFA

Shirikisho la Soka Tanzania TFF limetangaza kuwa Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania U17 “Serengeti Boys” itashiriki kwenye mashindano maalumu ya maandalizi ya Afcon U17 yatakayofanyika Antalya nchini Uturuki mapema mwakani. Kikosi cha Serengeti Boys Kwa mujibu wa taarifa ya TFF kupitia tovuti yake, mashindano hayo yameandaliwa na Shirikisho la Soka barani  Afrika CAF kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA, ambapo yanatarajia kuanza Februari 22,2019 mpaka Machi 2,2019 na kushirikisha jumla ya timu 12 kutoka Afrika na Ulaya. Mbali na Serengeti Boys, nchi nyingine za Afrika zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Angola, Morocco, Cameroon, Uganda, Nigeria, Senegal na Guinea ambazo zitaungana na timu nne kutoka bara la Ulaya. Serengeti Boys imewasili nchini jana Desemba 17 ikitokea nchini Botswana ambako ilialikwa kushiriki mashindano ya mataifa ya kusini mwa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, ambako imefanikiwa kurudi na ubingwa w...

Aliyejaribu kuwauza watoto wake pacha akamatwa Nigeria

MTEULE THE BEST Mwaka 2013 wasichana wajawazito 17 na watoto 11 waliokolewa wakati polisi walivamia "kiwanda cha watoto" katika jimbo la Imo Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya madai kuwa alijaribu kuwauza watoto wake pacha wenye umri wa mwezi mmoja nchini Nigeria. Ameshtaki kwa kuhusika katika bishara ya kuuza watoto lakini polisi wanasema kuwa mashtaka zaidi yataongezwa. Mwanamke huyo alikamatwa wakati akijaribu kuuza watoto wake wasicha kwa dola 980 kwa mnunuzi ambaye aliwajulisha polisi. Visa vya kuuzwa watoto wa kupangwa vimekuwa tatizo kwa muda mrefu chini Nigeria. Nigeria ni mzalishaji mkuwa wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu milioni 170 wanaishi kwenye umaskini. Alipohojiwa mwanamke huyo alisema kuwa changamoto za kifedha zilisababisha afanye hivyo. Nigeria ni mzalishaji mkuwa wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu milioni 170 wanaishi kwenye umaskini. Mwaka 2013 wasichana wajawazito 17 na watoto 11 waliokolewa wakati polisi walivamia "kiwanda...