Wanawake wa Freemason wamekuwa wakikongamana kwa zaidi ya miaka 100 sasa - wakifanya matambiko na sherehe sawa na wenzao wa kiume. Lakini si watu wengi wanaofahamu kuwepo kwa kundi hili. Sasa tunaweza kukufahamisha zaidi kuhusu shughuli za Freemason hawa wa kike baada ya kipindi cha redio cha Victoria Derbyshire cha BBC kuruhusiwa kuzungumza nao. "Freemason ni nani?" anauliza mmoja wa viongozi wao ambao huitwa master (gunge) katika Kongamano Tukufu la Jumuiya ya Freemason wa Kale. "Ni mfumo wa kipekee wa maadili ambao umezingirwa na istiari na ishara zenye maana," anajibu Dialazaza Nkela. Nkela anashiriki katika sherehe ya kipekee ya kumfikisha ngazi ambayo hufahamika kama "shahada ya pili". Ni sherehe ya kusherehekea kupanda hadhi kwake katika kundi lake. Kufikia kwake "shahada ya kwanza" kuliadhimishwa kwa kuingizwa kwake katika kundi hilo, shughuli ambayo ilihusisha yeye kuweka wazi "mkono wake wa kulia, ziwa lake la kulia na goti l...