Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba 2, 2018

Waafrika Kusini waandamana kisa Makonda

Wananchi nchini Afrika Kusini wameandamana mpaka ubalozi wa Tanzania, wakipinga kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kukataza vitendo vya ushoga na usagaji kwenye mkoa wake. Wananchi hao ambao idadi yao haikujulikana kwa mara moja, pia wamemtaka Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuingilia kati suala hilo, ikiwezakana awape kibali wananchi hao (mashoga) ambao wametajwa kuwa maisha yao yapo hatarini, waweze kuishi Afrika Kusini. “ Rais Ramaphopsa, tunakuita ili utambue hali iliyopo sasa Tanzania, kunyanyaswa kwa haki za binadamu na uhuru wa binadamu, mwambie Makonda kuwa haukubali hiki kitu, tunakutaka uwape hifadhi watu hawa  wa Tanzania, ambao wapo katika hatari ya kuporwa uhuru wao, tunakutaka uchukue hatua kama katiba yetu inavyosema na kitendo chako cha kutetea haki za binadamu ”, walisikika waandamani hao kwenye ujumbe wao. Ikumbukwe kwamba hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alianzisha kampeni ya kukamata watu wanaojihusisha na...

Mfungwa achagua kuuawa kwa kutumika kiti cha umeme badala ya sindano ya sumu Marekani

The electric chair has gradually been replaced as the main method of execution Mfungwa mmoja katika jimbo la Tennessee nchini Marekani atauawa kwa kiti cha umeme baada ya kudai kuwa sindano ya sumu itasababisha ateseke. David Earl Miller, ambaye amekuwa kwenye hukumu ya kifo kwa miaka 36 ni kati ya wafungwa wanaoongezeka wanaojaribu kukwepa sindano ya sumu kufuatia visa kadhaa vya kufeli. Mfungwa mwingine huko Tennessee Edmund Zagorski, aliuawa kwa njia ya umeme mwezi uliopita. Kuuliwa kwa kutumia sindano ya sumu ndiyo njia kuu ya kuwaua wafungwa katika jimbo hilo. Hata hivyo wafungwa katika jimbo hilo ambao walitenda uhalifu kabla ya mwaka 1999 wataruhusiwa kuchagua kuuliwa kwa njia ya umeme. Mahakamani, Miller na Zagorski walitaja kisa cha kuuuliwa Billy Ray Irick cha mwezi Agosti ambaye alibadilika rangi kuwa Zambarau na kuchukua dakika 20 kufa. Kuuliwa kwa Zagorski ilikuwa mara ya pili kiti cha umeme kimetumiwa katika jimbo hilo tangu mwaka 1960. Miller alikutwa na ha...

Magufuli amgusia Lowassa kuhusu maji

Rais Dkt. John Magufuli amezungumzia kitendo cha Mbunge wa Monduli (CCM), Julius Kalanga kumuomba apeleke maji jimboni kwake ilihali jimbo hilo limewahi kuongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye pia amewahi kuwa waziri wa maji. Rais Dkt. Magufuli akiwa na Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Akizungumza na wananchi wa Arumeru, ambapo amezindua na kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa visima vikubwa vya maji zaidi ya 20 jijini Arusha, Rais Magufuli amesema kuwa anampongeza Kalanga kwa kuhamia CCM akitokea CHADEMA kwakile alichosema ni kitendo cha kijasiri. " Kalanga,  Mbunge wa Monduli aliwahi kuniomba maji akiwa CHADEMA, lakini amesahau kuwa Lowassa amewahi kuwa Waziri wa Maji, simsemi mzee wangu namaanisha kuwa uzalendo unaanzia nyumbani, nikupongeze Kalanga kwa ujasiri wako wa kurudi huku, maji utapata ", amesema Rais Magufuli Katika hatua nyingine amewaomba Watanzania kumuombea ili awatumikie vyema, " Muendelee kuniombea ili cheo changu cha Urai...

Rais John Magufuli leo Desemba 2, 2018 amezindua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa visima vikubwa vya maji zaidi ya 20 jijini Arusha.

Rais John Magufuli leo Desemba 2, 2018 amezindua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa visima vikubwa vya maji zaidi ya 20 jijini Arusha. Rais Dkt. John Magufuli. Rais amesema kuwa mradi huo utakaogharimu shilingi bilioni 520, unahusisha visima vya kuchimbwa na kumaliza tatizo la maji katika Jiji hilo, na zimekopwa katika Benki ya Maendeleo ya Afrika, hivyo zitalipwa na Watanzania wote kupitia kodi. " Serikali imekopa bilioni 520 kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika, kwa ajili ya Arusha ili kutekeleza mradi wa maji, hizi hela zitalipwa na Watanzania wote, na tumezileta kwa wale wale wanaoitukana serikali, na yote ni kwasababu maendeleo hayana chama ", amesema Rais Magufuli. Aidha Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Isack Kamwele kutosita kuwafukuza wakandarasi wakishindwa kutekeleza mradi huo kwa wakati, " Waziri usiogope kufukuza wakandarasi, kumbuka hata mimi nimewahi kuwa Waziri wa Ujenzi na sikusita kutimua wakandarasi wasiotekeleza miradi, w...