Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya ZIMBABWE

Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Idai yaongezeka kwa kasi nchini Msumbiji

Wafanyakazi wa shirika la uokoaji wakiwa wanajiandaa kuondoa miili kutoka kwenye helikopter Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na kimbunga Idai kilichoikumba eneo la kusini mwa Afrika zaidi ya juma moja lililopita,imeongezeka kwa kasi siku ya Jumamosi. Idadi ya waliothibitishwa kupoteza maisha nchini Msumbiji imeongezeka kutoka 242 mpaka 417,waziri wa ardhi na mazingira nchini humo Celso Correia ameeleza. Idadi hii mpya inafanya waliopoteza maisha Msumbiji, Zimbabwe na Malawi kufikia 700. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi. Kimbunga kimeua takribani watu 259 nchini Zimbabwe na Malawi 56.Watu walipoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko. Lakini Umoja wa mataifa limesema maafisa wataweza kutathimini madhara pale maji yatakapopungua. Maelfu ya watu wakiwa wanasubiri kuokolewa kutoka kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kusini mwa Afrika Ofisi ya Umoja wa mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinaadamu, OCHA imesema kuwa mto wa Buzi na ...

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

Rais Mnangagwa wa Zimbabwe aizuru Tanzania kukuza uhusiano

Rais Mnangagwa alikaribishwa rasmi na mwenyeji wake rais John Magufuli Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa yuko Dar es salaam katika ziara ya kwanza nchini humo tangu aingie madarakani. Ni ziara ya siku mbili ambayo imetajwa kulenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, mwenyeji rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na Rais Mnangagwa wamekubaliana kuimarisha biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo mawili yaliotajwa kuwa na udugu wa kihistoria. Mnangagwa amewasili asubuhi hii na kupokewa na rais Magufuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Akiwa Tanzania kiongozi huyo anatarajiwa kutembelea chuo cha kilimo alikosomea miongoni mwa wapiganjiaji uhuru waliotoka nchi za kusini mwa Afrika. Kukuza uhusiano wa Zimbabwe na Tanzania: Tanzania ilikuwa na jukumu muhimu katika mataifa ya Afrika yaliojikomboa dhidi ya utawala wa wazung...

Mnangagwa:Uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa

Mnangagwa amesema uchaguzi uko palepale Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amesema uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa tarehe 30 mwezi Julai, ingawa kulitokea alichokiita jaribio la kukatiza uhai wake lililotokea siku ya Jumamosi. Katika hatua nyingine, msemaji wa Polisi, Charity Charamba amevitaka vyombo vya habari na Umma kujitokeza iwapo wana picha za video za tukio la mlipuko wakati huu ambapo uchunguzi unafanyika. Amwewaambia wanahabari mjini Harare kuwa zawadi nono itatolewa kwa taarifa itakayotolewa kusaidia kwenye uchunguzi wao.Idadi ya waliojeruhiwa sasa imefika 49 na Polisi na idara za usalama ziko katika uwanja wa White City eneo ambalo mlipuko ulitokea. Watu walijeruhiwa kutokana na mlipuko uliotokea kwenye mkutano wa hadhara mjini Bulawayo, tukio lililotokea karibu kabisa na Mnangagwa wakati akiondoka jukwaani. Maafisa wamesema masuala ya usalama yataangaliwa tena. mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa ni wa kwanza tangu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo R...

Mnangagwa anusurika jaribio la mauaji

Picha za televisheni ya shirika la utangazaji la Zimbabwe zimeonesha mripuko mkubwa kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa ukihutubiwa na Rais Emmerson Mnangagwa katika kile kinachotajwa kuwa jaribio la mauaji dhidi yake. Msemaji wake, George Charamba, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba rais huyo mwenye umri wa miaka 75, ambaye kwenye mkutano huo alikuwa ameambatana na makamu wake wawili, yuko salama kwenye ikulu ndogo mjini humo. "Rais ameondoshwa akiwa salama. Yuko kwenye nyumba ya serikali ya Bulawayo. Tunashukuru kwamba ulikuwa ni mripuko, na kwa hakika ulitokezea karibu sana na jukwaa kuu," alisema Charamba. Shahidi mmoja ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba mripuko ulitokea muda mchache baada ya Mnangagwa kumaliza hotuba yake na wakati akiondoka jukwaani. Picha zilizotumwa mitandaoni zinamuonesha kiongozi huyo akiwapungia mkono wafuasi wake, akinyanyua hatua kuondoka jukwaani na kuanza kutembea kutoka meza kuu, ambapo sekunde...

Itai Dzamara: Mwanamume aliyempinga Robert Mugabe na akatoweka

Dzamara Itai Dzamara mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Robert Mugabe kabla hajatoweka. Miaka mitatu baadaye wapendwa wake bado wanasubiri majibu. Sheffra Dzamara hajamuona mume wake kwa zaidi ya miaka mitatu. Maisha yake yalibadilika ghafla tarehe 9 Machi mwaka 2015 wakati Bw Dzamara alitekwa nyara. Tangu wakati huo ameishi maisha yaliyojaa giza pasipo kujua ikiwa yuko hai au amekufa. 'Huwa ninatabasamu' Licha ya kutokuwepo kwake Bw Dzamara bado yuko chumbani walimokuwa wakiishi kwenye mtaa unaojulikana kama Glen Norah huko Harare. Sehemu moja ya nyumba yao kuna picha yake. Kwenye picha hizo Bw Dzamara na mke wake wanaonekama wakitabasamu, ishara ya vile siku zao zilikuwa nzuri,. Maisha tangu mumuwe atoweka hajakuwa rahisi. "Kwa kusema ukweli ninahisi mpweke," Bi Dzamara anasema. Hata hivyo ni lazima aonyeshe sura ya ujasiri kwa mtoto wao wa kiume wa miaka 10 na msichana wa umri wa miaka mitano. "Wakati sina raha wanafah...

Wizi wa almasi: Mugabe atakiwa kutoa ushahidi

Bunge la Zimbabwe limemtaka rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe kutoa ushahidi wa madai aliyotoa kuhusu wizi wa almasi. Bunge la Zimbabwe limemtaka rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe kutoa ushahidi wa madai aliyotoa kuhusu wizi wa almasi. Bwana Mugabe alizishutumu kampuni za kigeni za kuchimba madini kwa ''kuiba'' na ''kusafirisha'' katika mahojiano na runinga ya taifa 2016. ''Kampuni hizo zimetuibia utajiri wetu'' , alisema. Akiongzea kuwa wizara ya fedha ilipokea $15bn pekee. Haijulikani iwapo raia huyo mwenye umri wa miaka 94 atakubali kufika mbele ya kamati hiyo ya bunge. Alilazimishwa kujiuzulu mwezi Disemba iliopita kufuatia mapinduzi ya kijeshi na bado anahudumiwa na serikali kama rais wa zamani

Mugabe aondoka Zimbabwe tangu kuondolewa madarakani

MTEULE THE BEST Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameondoka nchini humo kwa mara ya kwanza tangu alipoondolewa madarakani na jeshi. Bw Mugabe amesafiri kwenda Singapore kwa matibabu. Kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa serikali ambao wamezungumza na Reuters, Mugabe, 93, aliondoka nchini humu kwa ndege kutoka mjini Harare. Aliandamana na mke wake Grace na wasaidizi kadha. Anatarajiwa kutua mjini Malaysia ambapo binti Bona yupo akiwa mjamzito. Mugabe, aliyekuwa ameongoza taifa hilo kwa miaka 37, alijiuzulu baada ya jeshi likishirikiana na baadhi ya maafisa wakuu wa chama tawala cha Zanu-PF kumgeuka ilipobainika kwamba alikuwa anamuandaa Grace, 52, awe mrithi wake. Safari hiyo ina maana kwamba Mugabe huenda hatakuwepo nchini Zimbabwe chama cha Zanu-PF kitakapokuwa kinamuidhinisha rasmi Rais Emmerson Mnangagwa kuwa kiongozi wa chama na mgombea urais wa chama hicho uchaguzi wa mwaka ujao. Chama hicho kinatarajiwa kuandaa mkutano wake mkuu wikiijayo. Maafisa wa usalama ha...

Ulinzi mkali Nairobi Kenyatta akitarajiwa kuapishwa

Ulinzi umeimarishwa katika jiji kuu la Kenya, Nairobi pamoja na miji mingine mikuu Rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuapishwa kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine hapo kesho. Muungano wa upinzani umetangaza kwamba hautambui sherehe hiyo na haumtambui Bw Kenyatta kama rais aliyechaguliwa na wananchi. Kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga amepanga kuandaa mkutano mkubwa wa kuwakumbuka watu waliofariki wakati wa makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na polisi. Bw Odinga na muungano wake wa National Super Alliance (Nasa) wamesisitiza kwamba mkutano huo utafanyika katika uwanja wa Jacarada, Nairobi, takriban kilomita kumi hivi kutoka uwanja wa Kasarani ambapo sherehe ya kuapishwa kwa Bw Kenyatta itakuwa inaendelea. Polisi hata hivyo wamesisitiza kwamba hakutakuwa na mkutano mwingine Nairobi ila sherehe ya kumuapisha Bw Kenyatta. Bw Odinga alisusia uchaguzi wa marudio uliofanyika 26 Oktoba baada ya kufutiliwa mbali kwa uchaguzi wa kwanza uliokuwa umefanyika tarehe 8 Agosti. Mahakam...

Mugabe apewa sikukuu ya taifa Zimbabwe

Haki miliki ya pichaAFPImage captionMugabe alikuwa ameongoza Zimbabwe tangu uhuru 1980 Serikali ya Zimbabwe imetangaza siku kuu mpya ya kukumbuka mchango wa Robert Mugabe ambaye aliondolewa madarakani wiki iliyopita. Gazeti la serikali la Herald limesema sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Bw Mugabe kila mwaka. Uamuzi wa kusherehekea Siku ya Taifa ya Vijana ya Robert Gabriel Mugabe kila 21 Februari ulifanywa rasmi kupitia tangazo rasmi kwenye gazeti la serikali. Mugabe: Mambo 5 unayopaswa kuyafamu Mugabe huwa anapumzisha macho si kulala Je Robert Mugabe ni nani? Tangazo hilo lilichapishwa Ijumaa - siku ambayo Rais Emmerson Mnangagwa aliapishwa kuwa rais, na kufikisha kikomo uongozi wa Mugabe wa miaka 37. Serikali ya Bw Mugabe ilikuwa imeamua kutangaza siku ya kuzaliwa kwake kuwa sikukuu ya taifa mwezi Agosti, baada ya kampeni kutoka kwa mrengo wa vijana katika chama cha Zanu-PF. Image captionRaia walimshangilia rais Mpya wa Zimbabwe E...

Mugabe 'anaendelea vizuri'

Mpwa wa Robert Mugabe anasema kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe ana furaha na afya njema licha ya kulazimishwa kujiuzulu wiki hii Alikuwa ni mtu aliyependa sherehe kubwa ambazo zilikuwa zikiandaliwa mara kwa mara na chama tawala cha Zanu-PF Mpwa wa Robert Mugabe anasema kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe ana raha na afya njema licha ya kulazimishwa kujiuzulu wiki hii baada ya kutawala kwa miaka thelathini na saba. Leo Mugabe ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, kwamba alimtembelea mjombake ambaye anasema anaendelea vizuri baada ya utimuliwa kwake madarakani. Kauli ya Leo Mugabe inaashiria kiongozi huyo mkongwe amezoea kwa upesi kutimuliwa kwake kutoka uongoai wa taifa hilo. Amesema mjombake anatazamia maisha yake ya baada ya uongozi, ambayo yatajumuisha ukulima na kuishi katika nyumba yake mashambani. 'Grace, bado yupo naye' amesema Leo Mugabe akimaanisha mkewe rais huyo wa zamani. Ameeleza kuwa anashughulika na mipango ya kujenga chuo kikuu kwa heshima ya m...

Emmerson Mnangangwa ndiye rais mpya wa Zimbabwe

Umati mkubwa wahudhuria kuapishwa kwa Mnangagwa Emmerson Mnangagwa ameapishwa kama rais mpya wa Zimbabwe , huku kukiwa na miito ya kumtaka amalize "utamaduni wa ufisadi''. Emmerson Mnangagwa ameapishwa rasmi baada ya kurejea nyumbani kutoka uhamishoni Jumatano Raia wa Zimbabwe wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa michezo mjini katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa. Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla. Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ameapishwa katika uwanja michezo wa Harare. Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke . Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi". Taarifa ya kuondoka mada...

Kiongozi mpya wa Zimbabwe kuapishwa

Emmerson Mnangagwa alirejea kama shujaa Zimbabwe nchini Zimbabwe Jumatano Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla. Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ataapishwa kaka uwanja wa ndege wa Harare. Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke . Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi". Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku ya Jumanne iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe Ilitolewa kwa njia ya barua bungeni na kikao cha kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae kikakatizwa. Katika barua hiyo Bwana Mugabe alisema anajiuzulu ili kuruhusu mchakato rahisi na wa amani wa ukabidhianaji mamlaka na kwamba uamuzi wake ulikuwa wa hiari. Ra...

Je Robert Mugabe ni nani?

Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amejiuzulu Mwaka 1980, Bw Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake Mwaka 1987,alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake Uchumi ulidororeka baada ya mwaka 2000… Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara ya uchumi Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi Ndoa yake na Grace Mugabe ,anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza W...

Rais Robert Mugabe amejiuzulu

Katika dakika chache zilizopita , spika wa bung la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu Rais Robert Mugabe amejiuzulu Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu . Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha reuters. Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake. Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano. Raia wa Zimbabwe wafurahia kujiuzulu kwa Mugabe Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani. Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii. Amekuwa mamlakani tangu tai...

Zimbabwe: Emmerson Mnangagwa amtaka Mugabe ajiuzulu sasa

Makamu wa rais wa zamani, ambaye kufutwa kwake kazi kulisababisha jeshi kuchukua mamlaka ya nchi , amemtaka rais Robert Mugabe ajiuzulu mara moja. Rais Mugabe anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa umma na chama chake cha Zanu-PF Makamu wa rais wa zamani , ambaye kufutwa kwake kazi kulisababisha jeshi kuchukua mamlaka ya nchi , amemtaka rais Robert Mugabe ajiuzulu mara moja. Emmerson Mnangagwa amesema alitoroka nje ya nchi wiki mbili zilizopita wakati alipobaini kuwa kuna njama za kumuua na hatarejea nchini hadi atakapohakikishiwa usalama wake. Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuwa rais ajaye wa Zimbabwe Chama cha rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kinatarajiwa kuanza mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae. Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang'anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg'oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu. Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 "kumpa ...

Chama cha Zanu-PF kimemfuta Mugabe kama kiongozi wake Chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF kimefuta Robert Mugabe kama kiongozi wake.

Chama cha Zanu-PF kimemfuta Mugabe kama kiongozi wake Chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF kimefuta Robert Mugabe kama kiongozi wake. Kimemtua aliyekuwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa ambaye alifutwa wiki mbili zilizopita kama kiongozi wake. Kufutwa kwa Bw. Mnangawa kumezua mambo mengi huku jeshi likitwaa madaraka na kumzuia Mugabe 93, kumteua mke wake Grace kama makam wa rais. Maelfu ya watu nchini Zimbabwe waliingia barabarani siku ya Ijumaa kuandamana kumpinga Bw. Mugabe. Bw. Mugabe anatarajiwa kukutana na makanda wa jeshi na msafara wa magari umeonekana ukiondoka makao ya rais. Mkuu wa chama chenye nguvu cha wale waliopigania uhuru Chris Mutsvangwa, aliiambia Reuters kuwa chama kilikuwa kinaanza mchakato wa kumuondoa Mugabe madarakani kama rais.

Raia wajitokeza kumshinikiza Mugabe kujiuzulu Zimbabwe

Maelfu ya raia wa Zimbabwe wamejitokeza barabarni hasa mjini Harare wakijiandaa kwa mkutano mkubwa unaoungwa mkono na chama tawala ZANU-PF katika jitihada za kuongeza shinikizo za kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu,wakishikilia mabango yaliyoandikwa Mugabe Must Go. Zanu-PF ndio chama kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40. Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko mkubwa katika chama tawala. Kikubwa kinachozozaniwa ni nani atakayemrithi rais Mugabe atakapoochia madaraka. Jeshi la nchi hiyo lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina. MUgabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa madaraka. Zaidi ya hayo Bw. Mugabe angependa kuendelea kuwa u...

Mugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza

Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi Mugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano. Alihudhuria sherehe za kufuzu kwenye mji mkuu Harare. Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi. Jeshi lilisema Ijumaa kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazunngumoz hayo haraka iwezekanavyo. Mtu moja aliyeshuhudia alinukuliwa na Reuters akisema kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza. Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kmfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua ungonizi wa Zanu-PF na urais.

Mamba' ambaye amegeuka kumuuma Mugabe

Mnangagwa alisaidia kuongoza vita vya kupigania uhuru vya Zimbabwe na baadaye kuwa jasusi mkuu wa nchi wakati wa mgogoro wa ndani kwa ndani ambapo maelfu wa wananchi waliuwawa.   Mnangagwa amekuwa miongoni mwa waliotarajiwa kumrithi Mugabe Imekuwa siri ya wazi nchini Zimbabwe kwa miaka mingi kuwa Emmerson Mnangagwa angechukua nafasi ya Robert Mugabe na kuwa rais. Lakini Bwana Mugabe alionekana kucheza na hisia zake- wakati mwingine akimpandisha cheo ndani ya chama tawala cha Zanu- PF na serikalini na kuongeza tetesi ya yeye kuwa mrithi mtarajiwa lakini baadaye alishushwa cheo baada ya Mnangagwa kuonekana kuonesha nia zake mapema mno. Baada ya kutenguliwa, imeonekana kama subira ya mwanaume huyo maarufu kama "mamba" hatimaye imeisha. Baada ya Rais Mugabe kumtengua na kumshutumu kwa mfisadi, wafuasi wake na vikosi vya usalama waliingilia kati kwa niaba yake. Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe Constantino Chiwenga (kushoto) ni rafiki wa karibu wa Mnangagwa Mnangagwa ...