Mpwa wa Robert Mugabe anasema kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe ana furaha na afya njema licha ya kulazimishwa kujiuzulu wiki hii
Alikuwa ni mtu aliyependa sherehe kubwa ambazo zilikuwa zikiandaliwa mara kwa mara na chama tawala cha Zanu-PF
Mpwa wa Robert Mugabe anasema kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe ana raha na afya njema licha ya kulazimishwa kujiuzulu wiki hii baada ya kutawala kwa miaka thelathini na saba.
Leo Mugabe ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, kwamba alimtembelea mjombake ambaye anasema anaendelea vizuri baada ya utimuliwa kwake madarakani.
Kauli ya Leo Mugabe inaashiria kiongozi huyo mkongwe amezoea kwa upesi kutimuliwa kwake kutoka uongoai wa taifa hilo.
Amesema mjombake anatazamia maisha yake ya baada ya uongozi, ambayo yatajumuisha ukulima na kuishi katika nyumba yake mashambani.
'Grace, bado yupo naye' amesema Leo Mugabe akimaanisha mkewe rais huyo wa zamani.
Ameeleza kuwa anashughulika na mipango ya kujenga chuo kikuu kwa heshima ya mumewe ili kuwapa shughuli ya kufanya.
Hatahivyo, taarifa katika gazeti la Zimbabwe inatoa taswira tofauti ra rais huyo wa zamani - inasema Robert Mugabe alilia alipolazimishwa kujiuzulu Jumanne.
MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.
Maoni