MTEULE THE BEST
Nyota wa Brazil Neymar Jr amesema atajitoa kwa uwezo wake wote kuhakikisha taifa lake linashinda Kombe la Dunia mwaka 2018 kwenye fainali zitakazofanyika nchini Urusi.
Kikosi chetu kwasasa ni bora tofauti na ilivyokuwa mwaka 2014 tuliposhindwa kuchukua ubingwa tukiwa nyumbani, nitacheza kwa uwezo wangu wote kuhakikisha tunarejesha heshima ya kutwaa ubingwa wa dunia”, amesema Neymar.
Nyota huyo anayechezea PSG ya Ufaransa ameongeza kuwa timu yao ni bora ndio maana ilipoteza mechi moja tu kwenye michuano ya kuwania kufuzu fainali hizo kupitia kundi la Amerika ya Kusini (CONMEBOL).
“Kufuzu kwa kupoteza mechi moja tu kwenye kundi gumu la CONMEBOL ni hatua nzuri na imetufanya tujiamini na tutafanya vizuri na hayatajirudia mambo yaliyotokea kwenye fainali za miaka minne iliyopita”.
Kwenye fainali za Kombe la Dunia 2014, Brazil iliondolewa kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kichapo cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani ambayo iliibuka bingwa wa dunia kwa kuifunga Argentina kwenye mchezo wa fainali.
Maoni