Bondia, Ibrahim Class wa Tanzania
Bondia, Ibrahim Class wa Tanzania amepeperusha vyema bendera ya taifa baada ya kutetea ubingwa wake wa dunia katika uzito Mwepesi kwa kumtandika Koos Sebia wa Afrika kusini kwa alama katika pambano lilofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam .
Mgeni rasmi katika pambano hilo alikuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, ambaye amewataka vijana kote nchini kujiandaa vyema kabla ya kushiriki mchezo wowote kama wanataka kushinda kama alivyofanya Ibrahim Class.
Kwa upande wake Ibrahim Class amesema,ataendelea kucheza kwa bidii katika mapambano yake ili aendelee kutamba katika anga za kimataifa.
Maoni