Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa marefu lenye nguvu zaidi kupita yote duniani

MTEULE THE BEST



Korea Kaskazini imesema imefanikiwa kufanya jaribio la kombora la masafa marefu ambalo lina nguvu ya kushambulia eneo lolote Marekani. Jumuiya ya kimataifa imelaani vikali kurushwa kwa kombora lijulikanalo Hwangsong 15.

Jaribio hilo ndilo la kwanza kurushwa na Korea Kaskazini tangu mwezi Septemba na linakuja wiki moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuiweka nchi hiyo katika orodha ya nchi zinazotajwa kuuunga mkono ugaidi.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis amesema kombora hilo la hivi punde limeruka umbali mrefu zaidi na hivyo kumaanisha kuwa Korea Kaskazini inazidi kujiimarisha katika majaribio yake ya makombora. Kombora hilo la masafa marefu linasemekana kuruka juu na mbali zaidi kuliko makombora yaliyofanyiwa marekebisho kipindi cha nyuma.

Kombora lina nguvu kuliko yaliyopita

Kulingana na taarifa iliyosomwa katika kituo cha televisheni cha Korea Kaskazini, Kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un alishuhudia kurushwa kwa ufanisi kombora hilo lililopewa jina Hwansong 15 na kujivuna sasa wamekamilisha azma yao ya kihistoria ya kuwa dola lenye nguvu za kinyuklia.

Kiongozi wa Korea Kaskazini (Aliyesimama katikati) Kim Jong Un

Kombora Hwangsong 15 lina nguvu mara mbili ya lile lililorushwa mwezi Julai mwaka huu. Kituo hicho cha habari KCNA kilisema kuwa kombora hilo liliruka urefu wa kilomita 4,475 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 950 katika dakika 53 kabla ya kuanguka katika bahari karibu na Japan.

Nchi hiyo imesema inapenda amani na inaunda tu silaha za kinyuklia ili kujihami dhidi ya bepari Marekani na sera zake kandamizi za kinyuklia na vitisho vya mashambulizi ya kinyuklia kutoka kwa nchi hiyo.

Marekani, Japan na Korea Kusini zote zinakubaliana kuwa kombora hilo huenda ni la masafa marefu lakini wizara ya ulinzi ya Marekani imesema halikuwa kitisho kwa Marekani, maeneo wanayoyadhibiti wala washirika wake.

Trump na mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae In wameonya kuwa kombora lililorushwa na Korea Kaskazini ni kitisho kikubwa kwa dunia. Baada ya Trump na Moon kuzungumza kupitia njia ya simu, Taarifa kutoka kwa Ikulu ya Rais wa Marekani imesema viongozi hao wametilia mkazo kuwa uchokozi huo kutoka kwa Korea Kaskazini ni kitisho sio tu kwa Marekani na Korea Kusini, bali kwa ulimwengu mzima.

Trump asema wataishughulikia ipasavyo hali iliyojiri

Trump pia alizungumza na Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe kuhusiana na kitendo hicho cha Korea Kaskazini kurusha kombora licha ya kuwekewa vikwazo chungu nzima na Jumuiya ya kimataifa.

Rais wa Marekani Donald Trump

Japan na Korea Kusini zimetaka Korea Kaskazini kuwekewa shinikizo zaidi kuizuia kurusha makombora na kufanya majaribio ya silaha za kinyuklia. Marekani, Korea Kusini na Japan zimeitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baadaye Jumatano kujadili mzozo huo wa Korea Kaskazini.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani kurushwa kwa kombora hilo na kuitaka Korea Kaskazini kujiuzuia kufanya vitendo vitakavyosababisha msukosuko. China imesema inatiwa wasiwasi mkubwa kutokana na kitendo cha Korea Kaskazini kurusha kombora na kutoa wito pande zote kuwa na uvumilivu ili kudumisha amani na uthabiti.

Trump amewaambia wanahabari kuwa wataishughulikia ipasavyo hali iliyojitokeza na kwamba utawala wake hautabadili msimamo wake dhidi ya Korea Kaskazini ikiwemo kutaka iwekewe vikwazo zaidi ambavyo vitaathiri biashara zake. Kiongozi huyo wa Marekani na wa Korea Kaskazini wamekuwa wakirushiana cheche kali za maneno kwa miezi kadhaa sasa.

Marekani mara kwa mara imesema itatumia njia zote ikiwemo ya kijeshi kuikabili Korea Kaskazini lakini imesisitiza kwa sasa inapenda kutumia njia ya kidiplomasia. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema njia hiyo ya kidiplomasia bado iko wazi kwa sasa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...