MTEULE THE BEST
Mbunge wa Jimbo la arumeru Mashariki Joshua Nassari, amevamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha, na kunusurika kupigwa na risasi ambazo zimeua mbwa wake.
Kwenye ukurasa wake wa twitter Joshua Nassari ameandika ujumbe akitoa taarifa kuwa watu hao walivamia nyumbani kwake usiku wakiwa na silaha za moto ambazo waliwafyatulia mbwa wake, na yeye kunusurika baada ya kukimbia akiwa na mkewe, kitendo ambacho amesema kimemfanya akose imani na nchi yake.
"Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya Usa River usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu", ameandika Joshua Nassari.
Kufuatia tukio hilo East Africa Television ilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha kupata taarifa zaidi juu ya tukio hilo, na simu yake kuita bila mafanikio.
Maoni