RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ATEMBELEA BANDARINI, LEO JUMAPILI NOVEMBA 26,2017.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ATEMBELEA BANDARINI, LEO JUMAPILI NOVEMBA 26,2017.
_______________________________
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, mapema Leo Jumapili Novemba 26,2017, ametembelea na kukagua Sehemu ya Bandari na kukuta mrudikano wa magari zaidi ya 50, yanayodaiwa kuwa ni ya Polisi, na kwamba yaliagizwa na Ofisi ya Rais miaka miwili(02) iliyopita, tangu Juni,2015 na mtu asiyejulikana, huku Viongozi wote wakuu wa Mamlaka ya Bandari, POLISI, TAKUKURU, TRA na Vikosi mbalimbali wakikana kuyafahamu magari hayo.

Baada ya sintofahamu hiyo, Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amesema magari hayo yaliingizwa kinyemela nchini, kupitia uagizaji wa magari ya Polisi, na hivyo kuliagiza Jeshi la Polisi kuyatoa haraka, magari hayo, na kuwataka Mawaziri wake kushirikiana na kuwasiliana katika ufanyaji kazi wao.

......."Naomba haya magari ikibidi yagawiwe kwenye Mawizara ya Serikali ikibidi"........ Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, huku akimpa maelezo zaidi IGP,
........."IGP kwenye ofisi yako kuna madudu sana, ila nimekuweka wewe pale ili uyafukue na kuondoa madudu pale ofisini kwako hata kama ni rafiki yako"..............


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU