Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 29.11.2017













David Luiz



Real Madrid wanalenga kumsajili beki wa Chelsea na Brazil David Luiz 30 ambaye hatakikani katika uwanja wa Stamford Bridge msimu huu. (Daily Mail)

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anasema kuwa hajaelezwa iwapo atalazimika kuwasajili wachezaji wowote katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari iwapo mabingwa hao watetezi wanatarajiwa kuwafikia viongozi wa ligi Manchester City. (Guardian)



Leroy Sane

Mchezaji wa Manchester City na raia wa Ujerumani mwenye umri wa 21 Leroy Sane atapewa kandarasi mpya na Manchester City mwishoni mwa msimu huu. (Sun)

Watford wameonya kwamba mshambuliaji wao raia wa Brazil Richarlison, 20, ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano kutoka Fluminence mnamo mwezi Agosti kwa kitita cha £11m na anavutia klabu za Tottenham na Chelsea hauzwi wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (London Evening Standard)



Alexandro Sane

Chelsea wanatarajiwa kumnunua beki wa Juventus Alex Sandro ,26, mwezi Januari baada ya kushindwa kumsajili mshambuliaji huyo wa Brazil mwaka uliopita.(Daily Express)

Liverpool na Leicester wanaangazia kumsajili beki wa West Brom na Misri Ahmed Hegazi, 26, ambaye yuko katika mkopo kutoka klabu ya Al Ahly. (ESPN)



David Silva

Kiungo wa kati wa Manchester City David Silva, 31, anatarajiwa kuandikisha mkataba mpya ambao utamweka mchezaji huyo wa Uhispania katika uwanja wa Etihad hadi 2020. (Daily Mirror)

City haitamuuza mlinzi wa Ufaransa Eliaquim Mangala mnamo mwezi Januari , lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 hajapewa thibitisho kuhusu hatma yake katika klabu hiyo. (Goal)

Liverpool na Juventus wote wanataka kumsajili winga wa klabu ya Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 22 raia wa Ureno Gelson Martins. (A Bola, via Talksport)



Arsene Wenger

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Ivan Gazidis hausiki na mpango wa kuwanunua wachezaji kufuatia mabadiliko yaliofanyika katika klabu hiyo(Daily Mail)

Mchezaji anayesakwa na klabu ya Manchester City na Napoli Sime Vrsaljko anataka kuondoka Atletico Madrid. Beki hiyo huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Croatia anatafuta changamoto mpya(Talksport)



Antoinne Griezman

Mshambuliaji wa Atletico Antoine Griezmann angejiunga na Arsenal mwaka 2013 lakini the Gunners wakaamua kutomsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na wakati waliporudi kutaka kumsajili alikataa (Daily Express)

Swansea inapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Dominic Solanke, 20. (Wales Online)

Beki wa Arsenal na Ufaransa Laurent Koscielny, 32, anataka kumaliza mchezo wake katika klabu ya Lorient, kulingana na rais wa klabu hiyo ya Ufaransa (Canal+, via Goal)

Arsenal ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya ligi ya Uingereza wanaotaka kumsajili Novara Calcio mwenye umri wa 20 raia wa Uholanzi Alessio da Cruz. (Daily Mirror)



Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi,

Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, ambaye yuko Wolfsburg kwa mkopo hajui hatma yake katika klabu ya Anfield, huku mchezaji huyo wa Ubelgiji akiendelea kuvutia katika ligi ya Ujerumani ya Bundesliga. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Newcastle Alex Gilliead mwenye urmi wa miaka 21 ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Bradford, anatakiwa na klabu ya Hull, Millwall na wapinzani wao Sunderland. (Newcastle Chronicle)


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...