Muigizaji wa filamu za kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu ametangaza rasmi kurudi Chama Cha Mapinduzi huku akidai kwamba hawezi kuishi kwenye nyumba inayomkosesha amani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu amesema kwamba anatangaza rasmi kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambacho alitangaza kujiunga nacho Februari mwaka huu
"Siwezi Kuendelea kuishi kwenye nyumba inayo nikosesha amani... Peace of mind is everything for me. Natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi nyumbani" . Wema Sepetu.
MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.
Maoni