Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ni miongoni mwa viongozi mbali mbali duniani watakaohudhuria kuapishwa kwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mwenzake wa Tanzania John Pombe Magufuli
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ni miongoni mwa viongozi mbali mbali duniani watakaohudhuria kuapishwa kwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Katika taarifa iliotiwa sahihi na mkurugenzi wa idara ya habari, maelezo na msemaji mkuu wa serikali Hassan Abbas, Magufuli atajumuika na viongozi wengine katika kushuhudia kuapishwa kwa rais Kenyatta aliyeibuka mshindi katika uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 26 mwezi Novemba.
''Serikali inautaarifu umma kuwa rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe magufuli ataungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa mheshimiwa Uhuru Kenyatta kuwa rais wa kipindi cha awamu ya pili'', ilisema taarifa hiyo.
Iliongezea kwamba '' Muheshimiwa Kenyatta ataapishwa siku ya Jumanne Novemba 28 2017 jijini Nairobi baada ya ushindi alioupata katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini humo''
Maandilizi ya kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta siku ya Jumanne yamekamilika na usalama utawekwa kwa wale watakaoshiriki kulingana na kamati ya maandalizi.
Sherehe hiyo inatarajiwa kugharimu shilingi milioni 300 za Kenya huku ikidaiwa kuwa kiwango kikubwa cha fedha hizo kitawekwa katika kuimarisha usalama.
Mwaka 2013 wakati ambapo rais Kenyatta alikuwa akiapishwa kwa mara ya kwanza, kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo ilitaka kupewa shilingi bilioni 1.2 ambazo wizara ya fedha baadaye ilizipunguza na kufikia shilingi milioni 374 huku shilingi milioni 64 zikitolewa na idara ya mahakama.
Rais Magufuli ni rafiki wa karibu wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya ambaye alisusia uchaguzi huo Raila Amolo Odinga.
MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.
Maoni